kamishna msaidizi wa polisi Kaimu Kamanda wa jeshi la polisi ACP Isaa Suleiman akiongea na waandishi wa habari mkoani Iringa juu ya matukio mbalimbali yaliyojitokeza mkoani humo



Na Fredy Mgunda, Iringa.


JESHI la polisi mkoani Iringa linamshikilia Drive Tegete (23) kwa kosa kulawiti mtoto wa kiume mwenye umri wa miaka nane (08) baada ya kumrubuni akiwa anacheza mpira 

Kwa mujibu wa kamishna msaidizi wa polisi Kaimu Kamanda wa jeshi la polisi ACP Isaa Suleiman alisema kuwa kijana huyo alifanya tukio hilo kwenye shamba na Kisha kumuacha mtoto huyo 

"tulifanikiwa kumkamata mtuhumiwa aitwaye Drive Tegete miaka 23 mkulima mkazi wa kidamali kwa kosa la kulawiti mtoto wa kiume mwenye umri wa miaka nane jina lake linahifadhiwa baada ya kumrubuni akiwa anacheza mpira na watoto wenzake na Kisha kumpeleka kwenye shamba la magindi na kutenda tukio Hilo na kumuacha huko na kuondoka " Alisema ACP  Issa .

Kaimu Kanda ACP Issa alisema kuwa jeshi la polisi limefanikiwa katika kesi za mahakamani ikiwa ni pamoja na mshtakiwa Ayoub Msigwa kufungwa miaka 30 jela kwa kosa la kumfanyia ubakaji mtoto wa miaka 13 mwanafunzi wa darasa la sita .

"Tumepata mafanikio mbalimbali katika utekelezaji wa majukumu yetu kwa kesi za mahakamani  mshtakiwa Ayoub Msigwa kifungo Cha miaka 30 kwa kumfanyia ubakaji mtoto wa darasa la sita pia mshtakiwa Baraka Mwinuka kifungo Cha miaka 30 jela kutokana na kosa la kubaka , Emmanuel Gwandu amehukumiwa kifungo Cha maisha jela kwa kosa la kulawiti pia kuamriwa kumlipa mhanga wa tukio kiasi Cha shilungi millioni moja ,pia mtuhumiwa Wilbert mpyagisa amehukumiwa kifungo Cha miaka mitano jela kwa kosa la kuua bila kukusudia ,na mshtakiwa Nicolaus Nxavikr amehukumiwa kifungo Cha miaka mitatu jela kwa kosa la kujeruhi "

katika hatua nyingine ACP Issa Suleiman alisema walifanikiwa kuwashikilia watu sita kwa makosa ya kumiliki mali za wizi pamoja watuhumiwa wanne waliokutwa na silaha aina gobole sita na gololi zake kinyume na sheria 

" Jeshi la polisi tulifanikiwa kuwakamata watuhumiwa wanne ambao ni Mbomole Msaga miaka 73 mkristo mkulima mkazi wa kipera ,Angola Sanga miaka 33 mkristo mkulima mkazi wa kipera, Bahati Maliga miaka 33 mkristo mkulima mkazi wa kipera na Batrosi Kipako miaka 48 mkristo na mkazi wa ngomba kwa makosa ya kumiliki silaha aina ya gobore mbili pamoja na silaha mbalimbali za jadi ambazo ni panga moja kisi na goroli 10 zinazotumika kwenye gobore kinyume na sheria " Alisema ACP Issa Suleiman 

Aidha Kaimu Kamanda wa jeshi la polisi mkoani Iringa ACP Issa Suleiman amewataka baadhi ya wananchi walioibiwa mali zao kufika katika kituo Cha polisi ili kuzitambua mali zao ambazo zilikamatwa kwa watuhumiwa tofauti .
MWISHO.
Share To:

mwangaza wa hbari

Post A Comment: