Leo Mei 9, 2023 Katibu Mkuu Wizara ya Madini Kheri Mahimbali amekutana na kuzungumza na Washauri wa kodi kampuni ya PricewaterhouceCoopers Limited (PWC), Deloitte Tanzania na KPMG katika kikao kifupi kuhusu maandalizi ya Mpango Mkakati wa Miaka 10 wa Wizara ya Madini jijini Dar es Salaam.

Aidha, kikao hiki kimefuatia maelekezo ya Mhe. Waziri wa Madini Dkt. Doto Biteko aliyoyatoa hivi karibuni wakati akimtambulisha Katibu Mkuu kwa watumishi wa wizara ya Madini.

Kikao hicho kimezungumzia pia kuhusu shughuli mbalimbali za uchimbaji wa madini zinazofanyika na matarajio ya Sekta ya Madini katika kipindi cha miaka 10 ijayo 

Wengine waliohudhuria kikao hicho ni Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania  (GST) Dkt. Mussa Budeba, Mkurugenzi wa Sera na Mipango Augustine Ollal, Kamishna wa Msaidizi wa Madini Maruvuko Msechu, Mkurugenzi wa Ukaguzi na Biashara ya Madini Tume ya Madini Venance Kasiki na Kaimu Meneja Uwekezaji na Mipango STAMICO Nsalu Nzowa.

Share To:

Post A Comment: