Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Stellah Mutahibirwa, akiwakatika moja ya matukioya kikazi. Kamanda Mutahibirwa jana alizungumza na waandishi wa habari na kutoa taarifa ya baba kumuua mtoto wake kwa kumpiga na fimbo kichwani. 

Na Dotto Mwaibale, Singida

JESHI la Polisi mkoani Singida linamshikilia John Musoma (30) Mkazi wa Kijiji Cha Nkonko wilayani Manyoni kwa tuhuma za kumua mtoto wake na kumjeruhi mwingine kwa kumpiga fimbo kichwani.

Kamanda wa Polisi mkoani Singida, Stella Mutabihirwa, katika taarifa yake jana kwa vyombo vya habari, alisema mtuhumiwa huyo alikamatwa Mei 4, 2023 kwa kumuua mtoto wake aitwaye James Musoma (6) na kumjeruhi mwingine Joseph Musoma (8).

Kamanda Mutabihirwa alisema sababu za mtuhumiwa huyo kuwapiga watoto wake hao ni baada ya kuchelewa kufika shambani kufukuza ndege wanaoshambulia zao la iweke.

Alisema kutokana na tukio hilo mtuhumiwa atafikishwa mahakamani baada ya uchunguzi wa tukio hilo kukamilika.

Kamanda Mutabihirwa ametoa wito kwa wazazi na walezi kuacha vitendo vya ukatili vinavyoambatana na vipigo kwa watoto wao kwani vinaweza kugharimu maisha ya watoto.

Share To:

dotto mwaibale

Post A Comment: