KATAVI

TUME ya Madini Mkoa wa Katavi imeweka mikakati ya kudhibiti mianya ya utoroshaji madini kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Katavi hivyo, kuongeza kiwango cha makusanyo ya Serikali.


Mikakati hiyo imebainishwa na Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Katavi, Mhandisi Andrew Mwalugaja wakati wa mahojiano maalumu yaliyofanyika mkoani Katavi kwa lengo la kuandaa kipindi maalum na makala ya kuelimisha umma kuhusu Sekta ya Madini.


Mhandisi Mwalugaja ametaja mikakati hiyo kuwa ni pamoja na kuendelea kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama kuimarisha ulinzi maeneo ya migodi ili kudhibiti utoroshaji wa madini, hivyo Serikali kupata mapato yake stahiki hivyo Sekta ya Madini kuendelea kuwa na mchango mkubwa kwenye ukuaji wa uchumi wa nchi.


Kwa upande wake Mjiolojia wa Mgodi wa Katavi, Abrahman Said akielezea namna mgodi unavyotekeleza kanuni za ushirikishwaji wa watanzania katika Sekta ya Madini amesema kuwa mgodi umeajiri watanzania kwa asilimia 95 wakiwemo wanawake na wanaume pamoja na ushiriki wa uboreshaji wa huduma za jamii kwa kuchangia shilingi milioni 20 kwa ajili ya ujenzi wa darasa katika shule ya msingi Magula.


Share To:

ELIZA DOM

Post A Comment: