Mkuu wa wilaya ya Nachingwea Mohamed Hassan Moyo alipotembelea wanafunzi wa  shule ya sekondari Kipaumbele waliojeruhiwa na radi wakiwa darasani wanafanya mtihani wa kujipima wa wilaya ya Nachingwea
Mkuu wa wilaya ya Nachingwea Mohamed Hassan Moyo akiwafariji wazazi wa marehemu Alex Justine baada ya kujua kuwa mtoto wao amefariki kutokana na ajali ya Radi
Mkuu wa wilaya ya Nachingwea Mohamed Hassan Moyo alipotembelea wanafunzi wa  shule ya sekondari Kipaumbele waliojeruhiwa na radi wakiwa darasani wanafanya mtihani wa kujipima wa wilaya ya Nachingwea

Na Fredy Mgunda, Nachingwea.

MWANAFUNZI mmoja anayejulikana kwa jina la Alex Justine mwenye umri wa miaka 18 mwanafunzi wa kidato cha nne Kipaumbele sekondari amefariki baada ya kupigwa na radi akiwa darasani akifanya mtihani wa kujipima kwa ngazi ya wilaya.

Akidhibisha kutokea kwa kifo hicho mkuu wa wilaya ya Nachingwea Mohamed Hassan Moyo alisema kuwa ni kweli radi limesababisha kifo cha mwanafunzi mmoja anayejulikana kwa jina la Alex Justine na wengine 44  wamejeruhiwa.

Moyo alisema kuwa jumla ya wanafunzi wa kike wamejeruhiwa na wanaendeleza vizuri huku majeruhi wa kiume wakiwa 11 huku mmoja wao akifariki kabla ya kufikishwa Hospitali ya wilaya ya Nachingwea.

Kwa upande wake kaimu Mganga mkuu Dkt Ramadhan Maige alisema kuwa majira ya saa tisa na nusu alipokea simu kutoka kwa afisa elimu sekondari juu ya kutokea kwa ajali iliyotokana na radi.

Dkt Maige alisema kuwa walipokea majeruhi 45 kutoka katika shule ya sekondari Kipaumbele huku mwanafunzi mmoja akiwa tayari ameshafariki
Share To:

mwangaza wa hbari

Post A Comment: