Julieth Ngarabali. Pwani

 Zaidi ya  sh.470 milioni zimetengwa kwaajili ya shule mbalimbali za sekondari nchini zitakazofanikiwa kuunga mkono jitihada za Rais wa Jamuhuri ya Muungano  Samia Suluhu Hassan ya utunzaji mazingira na matumizi sahihi ya Nishati mbadala kwa  kupanda miti na kuitunza kwa asilimia 80.

Akizungumza Wilayani Kibaha  kwenye uzinduzi wa kampeni  ya utunzaji mazingira na matumizi ya nishati mbadala Kaimu Meneja wa benki ya NMB kanda ya Dar esalaam, Seka Urio  amesema fedha hizo zimetegwa na NMB kwa lengo la kuongeza chachu ya upandaji miti na utunzaji mazingira  hatua itakayochangia kurejesha uoto wa asili na kupambana na uharibifu wa mazingira unaobabishwa na vitendo vya ukataji miti hivyo.

Urio amesema fedha hizo zitatolewa kama zawadi kwa viwango tofauti kwa mshindi wa kwanza mpaka watatu pamoja na shule zote zitakazoshiriki kampeni hiyo nazo zitashikwa mkono ambapo zitapata sh.2 milioni pamoja na cheti cha ushiriki.

"Shule itakayopanda miti 2,000 na kuitunza ikakua  kwa asilimia 80 itaingia kwenye shindano na mshindi atazawadiwa sh 50 milioni na shule itakayopanda miti 1500 na kuitunza kwa asilimia 80 itazawadiwa sh 30.milioni na ya tatu ni Ile shule itakayopanda miti 1,000  na asilimia 70 ikakua vizuri itazawadiwa sh. 20 million "amesema kaimu meneja wa  NMB Kanda ya Dar esalaam

Naye mwakilishi  wa kampuni ya Taifa Gesi  ambao nao wanaendesha shindano Hilo Kwa vyomba vya habari na Kwa Halmashauri za Wilaya ,Angel Bhoke amesema kutokana na vitendo vya ukataji  miti vinavyofanywa na binafamu  kwa  shughuli mbalinbali ikiwemo kutengeneza mkaa vimekuwa vikisababisha upotevu wa miti ekari 400,000 kila mwaka kitendo ambacho ni hatari kwa mazingira.

"Sisi kwa upande wetu baada ya kuliona hilo tukaamua kuja na mpango wa kuzishindanisha  Halmashauri kuhusu upandaji miti na kwamba tutatoa zawadi kwa zitakazoshinda kutokana na vigezo tutakavyowaelekeza baadae"amesema Bhoke

Ametaja  kundi lingine litakalonufaika na mashindano hayo ni upande  wa waandishi wa habari nchini wa magazeti,TV na ,Radio ambapo masharti ni kuandika habari zinazotoa elimu kwa jamii ili kuongeza uelewa wa hasara zitokanazo na ukataji miti na kutambua matumizi ya nishati ya gesi kwa kupika.

"Mashindano yatafanyika kwa kipindi cha miezi mitatu kwa waandishi wa habari nchi nzima na baada ya hapo tutatoa zawadi na hili tunaamini itakuwa njia mojawapo ya kuelimisha jamii ili kutambua madhara yatokanayo na ukataji holela wa miti."amesema mwakilishi hiyo kampuni ya Taifa Gesi

Awali kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakari Kunenge , Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Nickson Saimon amesema  mkoa wa Pwani ni miongoni mwa mikoa ya Tanzania ambayo iliathiriwa na ukataji miti lakini kwa sasa wameendelea kufanya jitihada za kurejesha kwenye hali yake kwa kupanda miti kwenye maeneo mbalimbali.

"Mpaka sasa tumepanda miti 9.7 milioni na tumeendelea kupanda na hii ni moja ya mkakati ambao tumejiwekea ili kurejesha uoto wa asili"amesema

Mgeni rasmi kwenye uzinduzi wa kampeni hiyo Waziri  wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Raisi Muungano na Mazingira  Dk Selemani Jaffo ameuagiza uongozi wa kampuni ya Taifa Gesi kuzifungia mitambo ya gesi shule za sekondari za bweni na pia waende kwenye taasisi wazungumze nao namna ya kulipana  ili ziachane na matumizi  ya kuni kwa kupikia.

"Utafiti unaonyesha matumizi ya gesi gharama yake iko chini ukilinganisha na kuni mfano shule ya Sekondari Ruvu kabla ya kuanza matumizi ya gesi walikuwa wanatumia sh.4 milioni kwa mwezi lakini kwa kutumia gesi waliyounganishiwa na Taifa Gesi sasa wanatumia sh 2 milioni kwa mwezi"amesema Dokta Jafo.

Share To:

Post A Comment: