Mfamasia Mkuu wa Serikali Bw. Daudi Msasi akizungumza leo Aprili 5,2023 jijini Dodoma  kwenye semina ya Wahariri ya siku mbili iliyoanza leo ambayo imeratibiwa na Bohari ya Dawa(MSD) kwa wahariri wa vyombo vya habari nchini wakati akifafanua kuhusu Serikali kupitia Bohari ya Dawa (MSD) kununua mashine 140 kwa ajili ya kusafisha damu kwa wagonjwa wa figo,ambapo amesema kuwa gharama za kusafisha damu kwa wagonjwa hao itaendelea kupungua.

Meneja Uhakiki na Udhibiti Ubora  wa Bohari ya Dawa (MSD), Mwanashehe Jumaa akitoa akizungumza leo Aprili 5,2023 jijini Dodoma  kwenye semina ya Wahariri ya siku mbili iliyoanza leo ambayo imeratibiwa na Bohari ya Dawa(MSD) kwa wahariri wa vyombo vya habari nchini wakati,kuhusu ufangaji wa mashine ya kusafisha damu kwa wagonjwa wa figo katika vituo vitano.

Meneja Mawasiliano na Uhusiano Bohari ya Dawa (MSD) Eti Kusiluka akitoa maelekezo mafupi wakati  semina ya siku mbili ya  Wahariri wa Vyombo habari nchini leo  Aprili 5,2023 jijini Dodoma ikiendelea.


 Na Said Mwishehe

MFAMASIA Mkuu wa Serikali Daud Msasi amesema Serikali kupitia Bohari ya Dawa(MSD) imeshanunua mashine 140 kwa ajili ya kusafisha damu kwa wagonjwa wa figo, hivyo gharama za kusafisha damu kwa wagonjwa hao itaendelea kupungua.

Akizungumza leo Aprili 5,2023 kwenye semina ya wahariri wa vyombo vya habari iliyoandaliwa na MSD, Mfamasia Mkuu wa Serikali amesema  tayari kati ya mashine hizo  zimeshasambazwa kwenye hospitali 14 na mashine tano zimeshafungwa na kuanza kufanya kazi.

Amezitaja Hospitali zilizowekwa mashine hizo ni Chuo Kikuu Cha Dodoma( UDOM) Hospitali ya Rufaa  Amana, Hospitali ya Rufaa ya Kanda Chato, Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Pwani Tumbi, Hospitali ya Rufaa ya Mkoa SekouToure."Rais wetu  Dkt Samia Suluhu Hassan katika kipindi chake cha miaka miwili ameipa kipaumbele MSD na kusababisha isambaze Dawa kwa wakati na ubora" amesema Msasi.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa MSD Tukai Mavere amesema awali gharama ya huduma hiyo ilikuwa kubwa kutokana na ukosefu wa vifaa na tayari serikali imeleta mashine 140 kwa ajili ya kazi hiyo na zimesambazwa kwa ajili ya kuanza kutoa huduma hiyo.

Amesema kabla ya kuletwa kwa mashine hizo, ni hospitali tatu tu nchini za Muhimbili, Bugando na KCMC ndizo zilikuwa zikitoa huduma hiyo na hivyo kuchangia gharama zake kuwa kubwa zaidi na wananchi wengi kushindwa kumudu.

Meneja Uhakiki na Udhibiti Ubora ubora wa MSD, Mwanashehe Jumaa, amesema licha ya hospitali hizo kufungiwa mashine hizo katika vituo vitano,  tayari  taasisi hiyo imeshafanya ukaguzi katika vituo vingine vinne zaidi vya kutolea huduma na vipo tayari kufungiwa mashine hizo wakati wowote kutoka sasa.

Amevitaja  vituo vingine kuwa ni pamoja na Hospitali ya Mkoa wa Dodoma, Hospitali ya Mkoa wa Lindi, Hospitali ya Mawenzi iliyopo mkoani Kilimanjaro na hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro.

"Kila kituo kinatarajia kupokea mashine 10 za kusafisha damu, na kuna vituo vingine vitano vilivyobaki ambavyo tunaandaa mazingira rafiki kwa ajili ya kufunga mashine hizi, hii itasaidia sana kupunguza gharama kwa wagonjwa.Kwa wiki mgonjwa hulazimika kusafisha figo angalau mara tatu, lakini wengine walishindwa kutokana na umbali pamoja na gharama,"amesema Mwanashehe

Share To:

Post A Comment: