Wanawake watumishi wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mkoa wa Singida wakionesha furaha yao kabla ya kwenda kupanda miti kwenye chanzo cha maji cha Mwankoko kilichopo nje kidogo ya Manispaa ya Singida ikiwa ni shamra shamra kuelekea kilele cha Siku ya Wanawake Duniani, kesho Machi 08,2023. 

Na Dotto Mwaibale, Singida

 

WANAWAKE watumishi wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) na wenzao wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Singida (SUWASA) katika kuelekea kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani Machi 08, 2023, wamepanda miti katika chanzo za maji cha Mwankoko kilichopo nje kidogo ya Manispaa ya Singida ikiwa ni moja ya kazi ya upandaji miti ili kuimarisha uoto wa asili utakaosaidia upatikanaji wa mvua na hivyo kuimarisha vyanzo vya maji kwa ajili ya kuzalisha umeme mwingi.

Mbali na upandaji miti wanawake hao wa TANESCO wametoa msaada wa unga, mafuta ya kula, sabuni na vitu vingine kwa watoto yatima wa Kituo cha Upendo Home for Street Children, ikiwa ni shamrashamra kuelekea maadhimisho ya siku hiyo ambayo duniani kote yatafanyika kesho.

Zoezi hilo la upandaji miti limefanyika leo Machi 7, 2023 kwa kuwashirikisha wakuu wa idara wa taasisi hizo mbili za Serikali mkoani hapa. 

Akizungumza katika zoezi hilo la upandaji miti Afisa Uhusiano na Huduma kwa Wateja wa  Shirika hilo, Lulu Silungwe alisema TANESCO imekuwa ikitegemea mvua inayotokana na miti kwa ajili ya kusambaza huduma ya umeme hivyo zoezi hilo la upandaji wa miti litasaidia kukabiliana na athari za kimazingira na mvua kuwa nyingi. 

“Tumekutana hapa leo na wenzetu kutoka SUWASA kwa ajili ya kupanda miti chanzo cha maji Mwankoko chini ya kauli mbiyu yetu isemayo Panda Miti, Mvua Ndi, Umeme Ndindindi ikiwa ni moja ya kazi yetu kuelekea maadhimisho ya kilele cha Siku ya Wanawake Duniani ambayo ni kesho” alisema Silungwe. 

Alisema mbali ya kupanda miti pia watawatembelea watoto Yatima wanaolelewa Kituo cha Upendo Home for Street Children, kwa ajili ya kuwapatia zawadi mbalimbali ikiwa ni kazi yao nyingine kuelekea maadhimisho hayo. 

Neema Ntandu ambaye ni mfanyakazi wa shirika hilo alisema wamepanda miti 150 ya aina mbalimbali na kuwa watahakikisha inakuwa na kuimarisha chanzo hicho cha maji cha Mwankoko. 

Mwenyekiti wa Wanawake wa Shirika hilo Mkoa wa Singida, Asiatu Mnanura akizungumza wakati wa kutoa msaada kwa watoto wa kituo hicho alisema wamefurahi kuwatembelea ukizingatia kuwa wao ni wazazi hivyo waliona vizuri jambo hilo liwe ni sehemu ya moja ya kazi yao kuelekea maadhimisho hayo. 

Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Utawala wa SUWASA, Fatina Mbaga alisema ni wajibu kwa kila mwana Singida kupanda miti kwa wingi ili kuhifadhi mazingira jambo litakalosaidi kuhifadhi mazingira na kuwepo kwa mvua nyingi na hivyo kuwa na maji ya kutosha. 

Mratibu wa kituo hicho Afesso Ogenga alishukuru kwa msaada huo na kueleza kuwa kituo hicho kinawapokea watoto kutoka mitaani na majumbani lakini ni baada ya kufanyika utaratibu wa kuwatambua na kujua historia zao kwa kushirikiana na watu wa ustawi wa jamii.

Furaha ikiendelea kutamalaki kwa wanawake hao watumishi wa Tanesco Mkoa wa Singida.

Wanawake watumishi wa Tanesco Mkoa wa Singida wakifanya maandamano kuelekea katika zoezi hilo la kupanda miti.

 Mratibu wa Kituo cha  Home for Street Children, Afesso Ogenga akizungumza baada ya kukabidhiwa msaada huo.

Wanawake watumishi wa Suwasa Mkoa wa Singida wakipanda ngazi kuingia kwenye gari tayari kwa safari ya kwenda kupanda miti.

Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Utawala wa Suwasa, Fatina Mbaga, akizungumzia kuhusu zoezi hilo la upandaji miti.
Wanawake watumishi wa shirika hilo wakiwa wameshika miche ya miti tayari kwa kuipanda.
Kaimu Meneja wa Tanesco Mkoa wa Singida, Mhandisi , Ramadhan Mwanga akipanda mche wa mti eneo la chanzo cha maji Mwankoko.
Miche ya miti ikipandwa kwenye chanzo hicho cha maji.
Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Utawala wa Suwasa, Fatina Mbaga, akipanda mche wa mti.
Afisa Rasilimali Watu wa Tanesco Mkoa wa Singida, Angelina Kaarata (kulia) na Afisa wa shirika hilo, Neema Ndaskoy wakipanda mche wa mti katika eneo hilo., 
Yusra Nicholaus akipanda mche wa mti.
Salama Juma akipanda mche wa mti kwenye chanzo hicho cha maji.
Neema Ntandu ambaye ni mfanyakazi wa shirika hilo, akizungumzia umuhimu wa kupanda miti katika vyanzo vya maji.
Picha ya pamoja wakati wa kukabidhi msaada kwa watoto Yatima wa Kituo cha 
Zawadi kwa kituo hicho cha Yatima zikitolewa.
 

Share To:

dotto mwaibale

Post A Comment: