Jeshi la Polisi mkoa wa Iringa limeendelea kutoa elimu ya usalama barabarani Iringa kwa wanafunzi wa shule ya msingi Azimio
Jeshi la Polisi mkoa wa Iringa limeendelea kutoa elimu ya usalama barabarani Iringa kwa wanafunzi wa shule ya msingi Azimio
Jeshi la Polisi mkoa wa Iringa limeendelea kutoa elimu ya usalama barabarani Iringa kwa wanafunzi wa shule ya msingi Azimio

Na Fredy Mgunda, Iringa.


JESHI la polisi kitengo cha usalama barabarani Iringa limetoa elimu ya usalama barabarani katika shule ya msingi Azimio ili kupunguza ajali zinazowakumba watoto.

Akizungumza na wanafunzi hao mkuu wa kitengo cha usalama barabarani mkoa wa Iringa  MOSI NDOSELO Amewaasa watoto kutembea kwa umakini wawapo barabarani pamoja na kuacha kucheza barabarani kwani watoto wengi kuanzia miaka mitano wamekuwa wakipoteza maisha kutokana na ajali za barabarani huku wengine wakipata ulemavu wakudumu.


Kwa upande wake mkuu wa kitengo cha dawati la jinsia Elizabeth swai amewaasa watoto kujilinda dhidi ya vitendo vya ukatili kama ubakaji,ulawiti, mimba zautotoni na ajira za utotoni


Amewataka  watoto kutokumuamini mtu yoyote kwani ukatili unaweza kufanywa na mtu yoyote kama baba  kaka mjomba.

"Watu wanaotufanyia ukatili ni wale wanao tuzunguka" 

Pia amewasihi  watoto kuacha kutembea nyakati za usiku kutokana na matukio mngi ya ukatili kufayika katika nyakati hizo.


"Msipende kutembea usiku  ukitembea usiku unaweza kubakwa kulawitiwa unaweza pia kukatwa viungo"


Kamanda wa Jeshi la polisi mkoa wa Iringa ALAN BUKUMBI amesema kuwa iringa imekuwa  na matukio ya ujatili hasa kwa watoto ikiwemo watoto kupewa adhabu kubwa kubakwa na kulawitiwa.

Amesema wazazi hawafuatilii maendeleo ya watoto wao na hivyo kuwalea kinyume na maadili “Pamoja na kushughulikia makosa haya kumekuwa na changamotombalimbali zinazo wakumba watoto ambazo ni malezi duni kutoka kwa wazazi”

Amesema mzazi atakayebainika anamruhusu mwanae kwenda kwenye maeneo ya kucheza ya bahati na sibu maarufu  gulugulu, atachukuliwa hatua za kisheria.


 Nae Nogela Ndungulu ambae ni mwalimu mkuu wa shule hiyo wamepikea matukio ya watoto kuchomwa moto na wazazi kujilea, kukosa uangalizi na kupelekea watoto kujimudu katikati ukuaji wao wakiwa shuleni.

Share To:

mwangaza wa hbari

Post A Comment: