Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi (CCM) Mkoa wa Iringa Daud Yassin akiongea na kutoa maagizo saba kwa viongozi ambayo yanatakiwa kufanyiwa kazi 
Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi (CCM) Mkoa wa Iringa Daud Yassin akiongea na kutoa maagizo saba kwa viongozi ambayo yanatakiwa kufanyiwa kazi 
Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi (CCM) Mkoa wa Iringa Daud Yassin akitoa cheti kwa mwenyekiti wa chama cha mapinduzi CCM Iringa vijijini Costantino Kiwele wakati wa Halmashauri kuu ya chama cha mapinduzi wilaya ya Iringa vijijini na kutoa maagizo saba ambayo yanatakiwa kufanyiwa kazi 


Na Fredy Mgunda, Iringa.


Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Iringa Daud Yasin amepata nafasi ya kuzungumza na Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Iringa Vijini ikiwa ni ufunguzi wa uongozi kwenye Wilaya hiyo.

Pia ametumia nafasi hiyo kuupongeza uongozi wa CCM Iringa Vijijini  chini ya Mwenyekiti  Costantino Kiwele kwa kuandaa mafunzo hayo.

Katika ufunguzi wake uliofanyika leo Machi 15, 2023 katika Ukumbi wa CCM Mkoa wa Iringa, Ndugu Yasin ametoa maagizo saba muhimu.


Yassin alisema kuwa Wana CCM na wananchi waendelee kumuunga mkono Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kazi nzuri anazofanya za kuleta maendeleo na ustawi wa nchi yetu.

Alisema kuwa Wenyeviti wa Serikali za vijiji na mitaa kuhakikisha wanasoma mapato na matumizi ili wananchi waelewe jambo hilo.

Yassin alimtaka kila kiongozi  kutimiza wajibu wake kwenye nafasi aliyopewa dhamana na wananchi kwenye nafasi yake husika.

Alisema kuwa ni lazima kusikiliza na kutatua kero za wananchi kwenye ngazi husika ikiwemo vijiji.

Aliwataka Viongozi wa CCM kuhakikisha wanahudhuria vikao vya mashina kwenye maeneo yao ya ubalozi.

Lakini pia mwenyekiti Daud Yassin aliwaagiza walioanza kujipitisha kutojipitisha ili viongozi waliopo watekeleze majukumu yao na kamati husika ziwashughulikie kwa mujibu wa katiba.

Yassin alimalizia kwa kuwataka viongozi kuendelea kubuni miradi ya uchumi kwenye chama kuanzia ngazi ya mashina.

Alisema kuwa viongozi wanatakiwa kuhakisha utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM unasomwa.
Share To:

mwangaza wa hbari

Post A Comment: