Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Anthony Mavunde leo ametembelea na kuzungumza na wafanyabiashara wa soko la Majengo kusikiliza zao changamoto mbalimbali.

Akiwa hapo Mbunge Mavunde amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa maboresho makubwa ya miundombinu ya masoko ya Jijini Dodoma ambayo yatweka mazingira mazuri ya biashara kwa wafanyabiashara wakiwemo wafanyabiashara wa soko kuu la Majengo ambalo litafanyiwa maboresho makubwa. 

Akijibu Risala ya Wanakikundi wa MAVUNDE GARDEN MAJENGO ,Mbunge Mavunde ambaye pia ni Mlezi wa Kikundi hicho amechangia Tsh 2,000,000 kuongeza mtaji wa wanakikundi,amekabidhi pia viti 100 vya mradi wa kikundi,kuwanunulia shamba la ekari 2 kwa ajili ya mbogamboga na matunda,Bima ya Afya kwa ajili ya wanakikundi pamoja na kufunga TV kubwa ndani ya soko ili wafanyabiashara wapate fursa ya kupata habari mbalimbali.

Akitoa maelezo ya awali ,Diwani wa Kata ya Majengo Shifaa Ibrahim amemshukuru Mbunge Mavunde kwa kuwa nguzo kuu ya maendeleo ya soko kuu Majengo na kuahidi kuendelea kutoa ushirikiano katika shughuli za maendeleo katika soko na kata kwa ujumla.

Akishukuru kwa niaba ya Wafanyabiashara,Mwenyekiti wa Wafanyabiashara wa Soko Kuu Majengo Godson Rugazama amemshukuru Mbunge Mavunde kwa namna ambavyo msaada mkubwa katika kuboresha miundombinu ya soko na kuwawezesha wafanyabiashara kiuchumi kupitia fursa mbalimbali za mikopo hali ambayo imechochea kukua kwa vipato kwa wafanyabiashara hao.Share To:

Post A Comment: