Mjumbe wa baraza kuu la wazazi Taifa Mkoa wa Arusha Bi. Lilian Ntiro ametoa takribani matofali elfu moja 1000 huku akiahidi kutoa mifuko 50 mpaka 100 kwa ajili ya ujenzi wa Ofisi ya Jumuiya ya Wazazi wilaya ya Meru.

Bi. Liliana Ametoa Matofali alipoalikwa katika kikao cha Kamati ya Utekelezaji ya Jumuiya hiyo Meru hii ni kufuatia ahadi aliyoitoa wakati wa kampeni za uchaguzi wa chama cha Mapinduzi ambapo aliahidi kuchangia ujenzi wa ofisi.

“Nimekuja hapa leo kutengua ile ahadi yangu na siyo kwamba nitaishia hapa hapana bali nitakua nanyi bega kwa bega kuhakikisha ujenzi unakamilika na nitaanza na mifuko ya sementi 50 -100”.Alisema Bi.Ntiro

Wakati huohuo ametoa wito kwa viongozi wa  jumuiya ya wazazi kuzingatia maadili ya uongozi kwani uongozi siyo kiti bali ni kuwatumikia wananchi na kuinua jumuiya ya Wazazi.

Amesema kuwatumikia wananchi ni kutoa elimu kwa kuitisha mikutano mbalimbali pamoja na kusaidia makundi mbalimbali ya vijana wanaoharibikiwa kuacha makundi hayo na kufanya kazi kwa maslahi yao na Taifa kwa ujumla.

“Uongozi siyo kiti uongozi ni matendo na kazi zako kama umechaguliwa kamati ya utekelezaji alafu ukafikiri kiti kitakutumikia unakosea inatakiwa miaka yako mitano ukija kuomba kura nyingine  ueleze umefanya mikutano mingapi, Kitu ambacho kinatuvunja moyo na kuharibu jumuiya yetu ni Majungu,Fitna na kuwasema viongozi sasa tunatakiwa tuwaambie watu wetu kwamba tuwaheshimu viongozi wafanye kazi zao na nyie Viongozi kazi zionekane.”Alisisitiza Bi.Ntiro

Kwa upande wake Katibu wa Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Arusha Deogratius  Nakey Amesema mchango wa matofali elfu moja 1000 ni mkubwa sana hivyo kuwaasa Kamati ya utekelezaji mchango huo  ukatumike kwa kazi iliyopangwa.

“Naamini chini ya Mwenyekiti na Kamati yake ya utekelezaji sina mashaka kazi inaenda kufanyika kama Ilivyopangwa.”Alisema Share To:

Post A Comment: