Mwenyekiti wa Kamati ya Kuduma ya Bunge ya Miundombinu Mhe. Selemani Kakoso akiwa pamoja na Wajumbe wa Kamati hiyo kukagua ujenzi wa mradi wa barabara ya njia nane Kimara-Kibaha leo Machi 20,2023.

Mwenyekiti wa Kamati ya Kuduma ya Bunge ya Miundombinu Mhe. Selemani Kakoso akizungumza na Wajumbe wa Kamati hiyo pamoja na watumishi wa TANROADS mara baada ya kufanya ziara kukagua ujenzi wa mradi wa barabara ya njia nane Kimara-Kibaha leo Machi 20, 2023.

Mwenyekiti wa Kamati ya Kuduma ya Bunge ya Miundombinu Mhe. Selemani Kakoso akiwa kwenye kikao na Wajumbe wa Kamati hiyo pamoja na watumishi wa TANROADS mara baada ya kufanya ziara kukagua Mradi wa Ujenzi wa barabara ya njia nane Kimara-Kibaha leo Machi 20, 2023.

Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhandisi Godfrey Kasekenya akizungumza mbele ya Kamati ya Kuduma ya Bunge ya Miundombinu ikiongozwa na Mwenyekiti wake Mhe.Selemani Kakoso mara baada ya kamati hiyo kufanya ziara kukagua Mradi wa Ujenzi wa barabara ya njia nane Kimara-Kibaha leo Machi 20, 2023.

Mtendaji Mkuu wa TANROADS Mhandisi Rogatus Mativila akiwasilisha Utekelezaji wa Mradi wa Ujenzi barabara ya njia nane Kimara-Kibaha mara baada ya Kamati ya Kuduma ya Bunge ya Miundombinu kufanya ziara ya kukagua Mradi huo leo Machi 20,2023. Mjumbe wa Kamati ya Kuduma ya Bunge ya Miundombinu ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kilombero Mhe.Abubakar Asenga akichangia mapendekezo mara baada ya Mtendaji Mkuu wa TANROADS Mhandisi Rogatus Mativila (hayupo pichani) kuwasilisha Utekelezaji wa Mradi wa Ujenzi barabara ya njia nane Kimara-Kibaha. Wajumbe wa Kamati ya Kuduma ya Bunge ya Miundombinu wakimsikiliza Mtendaji Mkuu wa TANROADS Mhandisi Rogatus Mativila (hayupo pichani) wakati akiwasilisha Utekelezaji wa Mradi wa Ujenzi barabara ya njia nane Kimara-Kibaha mara baada ya Kamati ya Kuduma ya Bunge ya Miundombinu kufanya ziara ya kukagua Mradi huo leo Machi 20,2023.


KAMATI ya Kuduma ya Bunge ya Miundombinu yaishauri Serikali kupitia Wakala wa barabara Tanzania (TANROADS) kuanza na mfumo wa barabara zenye tozo katika mradi wa ujenzi wa barabara njia nane kutoka Kimara Jijini Dar es Salaam hadi Kibaha mkoa wa Pwani ili kuweza kuongeza mapato.

Ushauri huo umetolewa leo Machi 20,2023 wakati Kamati hiyo ilipofanya ziara kutembelea mradi wa barabara wa njia nane ambapo waliongozana na viongozi na watumishi kutoka Wakala wa barabara Tanzania (TANROADS) kuona Maendeleo ya Mradi huo ulipofikia pamoja na kuona changamoto zilizopo.

Akizungumza kwa niaba ya wajumbe wa Kamati hiyo, Mwenyekiti wa Kamati ya Kuduma ya Bunge ya Miundombinu Mhe. Selemani Kakoso amesema duniani kote, barabara nyingi zinajengwa kwa mfumo kama wetu ambao ulishaanza muda mrefu na sheria inatukataza huwezi kuwa na barabara ya tozo kama huna njia nyingine mbadala.

Aidha amesema katika mradi wa barabara kunatakiwa pia kuimarishwa kwa mifumo ya mifereji kwaajili ya majitaka kwani mvua zinaponyesha maji yanashindwa kwenda kwenye maeneo husika na kuleta kero kwa watumiaji wa barabara.

Pamoja na hayo Kamati hiyo imeridhishwa na miundombinu inayojengwa katika Mkoa wa Dar es Salaam na kuipongeza Wizara kwa usmamizi mzuri ambao wanaufanya kupitia TANROADS kujenga miundombinu ya barabara nchini.

"Tumeiona dhamira ya Serikali kupunguza msongamano ambao wanaamini utarahisisha shughuli nzima kwenye sekta ya uchukuzi". Amesema Mhe.Kakoso.

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi mhandisi Godfrey Kasekenya amesema kumekuwa na ongezeko la gharama kubwa kwenye ujenzi wa miundombinu kutoka kwenye gharama ya mwanzo mpaka mradi unapokaribia kuisha gharama zinaongezeka kutokana na usanifu wa ujenzi wa miundombinu mipya.

Nae Mtendaji Mkuu wa TANROADS Mhandisi Rogatus Mativila amesema mradi huo uliogharimu shilingi za kitanzania bilioni 218 umejengwa na Mkandarasi mzawa kutoka kampuni ya ESTIM CONSTRUCTION umefikia asilimia 98 na unatarajia kukamilika mwezi ujao.

Mhandisi Mativila amesema watahakikisha wanayasimamia kikamilifu maelekezo na ushauri ili kufikia matarajio yanayokusudiwa hasa katika uboreshaji wa miundombinu ya barabara.

Share To:

emmanuel mbatilo

Post A Comment: