Dkt .Tumaini Msowoya akizungumza na wazazi na wanafunzi katika mahafali ya 17 ya shule ya sekondari JJ Mungai wilaya mufindi mkoani Iringa.

Mgeni rasmi Dkt. Tumaini Msowoya akiwa katika picha ya pamoja na walimu wa kike wa shule ya sekondari JJ Mungai wilaya ya mufindi mkoani Iringa
Baadhi ya wanafunzi waliohitimu kidato Cha sita shule ya sekondari JJ Mungai wilaya mufindi mkoani Iringa.
Dkt. Tumaini Msowoya akikusanya fedha za harambee kwa wazazi wa wanafunzi wa kidato Cha sita kwa ajili ya kununua meza za kupatia chakula  bwaloni kwa wanafunzi


Na Fredy Mgunda, Iringa.

MJUMBE wa Kamati ya Siasa ya Halmashauri kuu Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Iringa Dkt.Tumaini Msowoya amewataka wahitimu wa kidato cha sita katika shule ya sekondari ya Jj Mungai kwenda kuwa mabalozi wema katika jamii baada ya kuhitimu masomo yao kwa kutoa elimu sahihi ya kukabiliana na mmomonyoko wa maadili na kupambana na ukatili wa kijinsia.

Akizungumza kwenye mahafali ya 17 ya wanafunzi wa kidato cha sita katika shule ya sekondari ya JJ Mungai alipomwakilisha Mkurugenzi wa Kampuni ya Qwihaya Mnec Leonard Mahenda,Mjumbe wa kamati ya siasa Halmashauri kuu ya chama cha mapinduzi CCM Dkt. Tumaini Msowoya alisema kuwa kutokana na uwepo wa mmomonyoko wa maadili kwa vijana wametakiwa kuwa mfano wa kuigwa  

 "Ndugu zangu wazazi kuna utafiti umetoka tarehe 26 /1/2023 utafiti huo unaonyesha kati ya vijana 10 ni kijana mmoja ndiye mwenye maadili tisa wote hawana maadili mi naomba tuangalie ukumbi huu saa hizi mkuu wa shule akiongea watoto wanatoka nje mziki ukipiga wanarudi ndani vipo vitu vinavutia sana tutenge muda wa kukaa na watoto wetu katika watoto kumi mmoja ndo anamaadili tunatakiwa tujiulize tunakwama wapi au wapi tunakosea zamani kuna kitu kilikuwa kinaitwa jicho la mama mama akikupiga jicho unajua tuu anataka maji ya kunywa sasa sisi tumekwama wapi eneo ambalo tumekwama natamani tujitafakari hasa kwenye malezi malezi sio walimu peke yao hawa walimu wakikusimulia wanayokutana nayo ukipewa darasa hata kidogo unashindwa" alisema Dr msowoya

Dkt . Tumain aliwataka wazazi kuzingatia suala la lishe ambalo kwa mkoa wa Iringa imekuwa changamoto kubwa kutokana na kushika nafasi ya pili kwa udumavu ambayo ni asilimia 56.9 kwa takwimu za mwaka 2023 

"Kuna watoto waliingia hapo wakaimba najua kuna watu hawajawasikiliza kwa sababu wakati ule sikuona kama mnaitikia sana walikuwa na ujumbe mzito sana wamewaomba wazazi sanasana walitoa ujembe wa ukatili wa kijinsia wazazi tunaomba muwalindw watoto nyumbani kwenu" alisema Dr Msowoya 

Kwa upande wa taaluma ya shuleni hapo Mkuu wa shule ya sekondari JJ Mungai Mwalimu Nashon Ndanzi amesema hali ya taaluma ni ya kuridhisha hivyo wanafunzi hao wameandaliwa vyema kwa ajili ya mtihani wao wa mwisho na kwamba hakuna mwanafunzi atakayefeli


Naye Mjumbe wa kamati ya shule aliwataka wanafunzi kuendeleza nidhamu na kuondokana na athari za mitandao ya kijamii na utandawazi ambazo zimeathiri jamii kwa kiwango kikubwa . 

Herieth Fumbe na Ivan  Maliva ni wahitimu wa kidato cha sita shule ya Sekondari ya JJ Mungai walisema kuwa wataitumia vizuri elimu waliyopatiwa pamoja na kukabiliana na changamoto za mmomonyoko wa maadili ambao umekithiri katika jamii . 

Wahitimu hao walieleza namna watakavyoenda kuwa mabalozi katika kupambana na mmomonyoko wa maadili huko mtaani sanjari na kupambana na ukatili wa kijinsia huku wakieleza namna walivyojiandaa na mtihani wao wa mwisho

Hata hivyo shule hiyo inakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa viti katika bwalo la kulia chakuala ambapo Dkt.Tumaini amechangia kiasi cha shilingi laki tano huku akiahidi kupeleka changamoto hiyo kwa mkurugenzi wa kampuni ya Qwihaya alyemwakilisha na anaimani changamoto hiyo itatatuliwa.

Shule ya sekonari JJ Mungai ilianzishwa mwaka 1984 iliyojengwa kama shule ya Jumuiya ya wazazi  huku ikifanya mahafali ya 17 ya kidato cha sita toka kuanzishwa kwake .

MWISHO .

Share To:

mwangaza wa hbari

Post A Comment: