Mjumbe wa Kamat ya Siasa ya Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Iringa,  Dkt Tumaini Msowoya akiwq kwenye picha na UVCCM kata ya Kihesa.
Mjumbe wa Kamat ya Siasa ya Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Iringa,  Dkt Tumaini Msowoya wa katikati akiwa makini kufuatilia mchezo ukiendelea


Na Fredy Mgunda, Iringa.


MJUMBE wa Kamat ya Siasa ya Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Iringa,  Dkt Tumaini Msowoya amewapongeza Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) Kata ya Kihesa, kwa kuandaa michuano ya mpira wa miguu kwa lengo la kusambaza ujumbe wa kupinga ukatili wa kijinsia.


Zaidi ya timu 20 zinashiriki kwenye michuano hiyo itakayomalizika kwa mshindi wa kwanza kutwaa kombe litakaloambatana na zawadi ya ng’ombe.


Akizungumza na vijana hao, Dkt Msowoya aliwataka wasichoke kuendelea kuwekeza kwenye soka ambako kuna vijana wengi wanaoweza kusaidia harakati za mapambano dhidi ya ukatili wa kijinsia.


“Ni kweli kwamba kata hii ya kihesa inamatukio mengi ya ukatili kwa watoto na wanawake, hongereni kuwekeza katika kutoa elimu lakini msichoke kufanya hivi,” alisema.


Awali, Mwenyekiti wa Kata ya Kihesa alisema baada ya kubaini matukio ya kijinsia kuwa mengi kwenye kata yao, waliamua kutumia michezo kama njia ya kupambana nayo.


Hata hivyo aliomba wadau kusaidia upatikanaji wa zawadi kwa ajili ya washindi, akidai kuwa ndio changamoto wanayokumbana nayo kwa sasa.

Share To:

mwangaza wa hbari

Post A Comment: