Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais menejimenti ya utumishi wa umma Deogratius Ndejembi,amesema kuwa Serikali imeishapeleka mtandao

katika maeneo mbalimbali hapa nchini  hivyo amezitaka taasisi binafsi
kuhakikisha kuwa zinafikisha vifaa vya kidijitali katika maeneo mengi
hususani vijijini.

Ndejembi ameyasema hayo alipokuwa akifungua kikiao
kazi cha siku tatu cha Serikali mtandao,kikao kilichowashirikisha
viongozi,watendaji na maofisa mbalimbali wa serikali,taasisi zake na
sekta binafsi.

Amesema kuwa lengo la serikali ni kuhakikisha kuwa mtandao unatomika
katika maeneo mengi hapa nchini ambapoamezitakataasisi za serikali
kutumia njia ya mtandao pindi wanapotekeleza majukumu yao au watoapo
huduma mbalimbali.Kwa upande wake katibu mkuu wa Wiza hiyo,Dkt.Laurian Ndumbaro amewaasa
wakuu wa taasisi kuhakikisha wanahama kwenda kwenye serikali mtandao
ili kurahisisha utoaji wa huduma kwa jamii na kuachana na matumizi ya
makaratasi.

“kuanzia sasa waku wa taasisi,idara na mashirika ya umma mnatakiwa
kujipanga kuhakikisha kuwa mnahama katika matumizi ya makaratasi na
kutumia jia ya serikali mtandao ili kurahisisha na kuharakisha utoaji
wa huduma.”alisisitiza dkt. Ndumbaro

Naye Mwenyekiti  wa bodi ya mamlaka ya serikali mtandao Dkt. Mussa
Kisaka akiziomba taasisi kuwa tayari kupokea mabadiliko ya kutumia
huduma ya serikali mtandao ambapo amewataka viongozi wote kusimamia
utekelezaji huo.

Amesema kuwa mafunzo ya mara kwa mara yanatakiwa kutolewa kwa
watumishi wa serikalina mashirikaya umma ili kupata uelewaa ufahamu wa
kutoha juuya mfumo huo.

Kwa upande wao baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo,Katibu tawala wa
Mkoa wa Katavi,Toba Nguvila na mkurugenzi wa halimashauri ya wilaya ya
Norongoro Jumaa mhina waliipangeza serikali kwa kuleta mfumo huo na
kusemakuwa utaongeza tija katikautoaji wa huduma.
Share To:

Post A Comment: