Naibu Waziri wa Maji Mhandisi Maryprisca Mahundi (Mb) ameiwakilisha Tanzania katika sherehe za miaka 17 ya Bonde la mto Nile Jijini Nairobi Kenya mkutano uliojumuisha nchi kumi kumi na moja wanachama.

Awali sherehe hizo zimetangauliwa na maandamo yaliyoongozwa na Brass Band ambapo mkutano huo umelenga kukabiliana na tabianchi sambamba na matumizi bora ya mto Nile(Nile Basin Inatiative).

 Katika hotuba yake Mudavadi amehimiza Mataifa wanachama kuhifadhi maji yanayotokana na mvua kwani wakati mwingine huleta migogoro katika nchi hizo za Afrika Mashariki.

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Maji Mhandisi Maryprisca Mahundi ambaye ni Mwenyekiti wa mkutano huo amepongeza Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kulipa ada zote za uanachama hivyo Tanzania kutokuwa na deni.

Aidha Mahundi amezitaka nchi wanachama kutunza mto Nile ili uwe endelevu na kusisitiza utoaji elimu kutunza mazingira na vyanzo vya maji ili maji ya mto Nile yatumike pia kuzalisha umeme na kilimo cha umwagiliaji

Share To:

Post A Comment: