Mbunge wa Jimbo la Monduli Fredrick lowassa Hii Leo amewasili Ofisi ya Mkuu Mpya wa Wilaya ya Monduli Kwa lengo la kumkaribisha DC mpya Selemani Mwenda katika Jimbo Hilo.

Katika utambulisho na ukaribisho huo mh Frederick Lowassa amempongeza DC Mwenda Kwa kuteuliwa Kuja Monduli pamoja na ziara alizozifanya ikiwemo ya kukutana na Viongozi WA Mila (malaigwanani) pamoja na Kuzindua kampeni yake ya upandaji wa miti.

"Nikupongeze sana DC wewe sio mgeni Monduli ni mtu ambaye tayari ulikuwa kwenye kazi hizi karibu Monduli naaahidi kukuunga mkono katika utekelezaji na usimamizi wa miradi lakini Nina maombi kwako ikiwemo swala la Maji tuna miradi mingi hapa lakini naomba ukazie wanamonduli wapate Maji, Elimu Monduli sisi ni vinara katika Elimu likazie hili katika Nafasi Yako, lakini pia Malisho kama Kuna technology ya uzalishaji wa majani basi watu wapatiwe elimu, pamoja kusimamia miradi mbalimbali" Amesema Mbunge Fredrick Lowassa.

Aidha Fredrick Amemuomba DC Mwenda kushiriki katika kuzindua / kutembelea Miradi mbalimbali zinazotekelezwa kupitia mfuko wa Jimbo.

Kwa Upande wake Mkuu wa Wilaya Ya Monduli Selemani Yusuph Mwenda Amemshukuru Mbunge huyo kwa kumtembelea na kumkaribisha Monduli na kuahidi kushirikiana kwa pamoja katika utekelezaji na usimamizi wa Miradi na kuahidi kuwa mkali kwa chochote ambacho hakitaenda sawa.

" Nashukuru kwa ukaribisho wako ,nilifika hapa nilipokelewa ila nilipata udhuru wako kutoka kwa katibu wako , na nilianza na Kikao Cha Malaigwanani, Wakuuu wa Idara kwa hiyo niseme hapa nina baraka zote za kufanya kazi, Nikuahidi TU kuwa pamona na wewe katika majukumu, Miradi mbalimbali na umezungumzia Mambo mengi ikiwemo Malisho, Barabara, Maji, Mfuko wa Jimbo,Elimu, usimamizi wa miradi , Monduli imekaa strategic sana kuhusu utalii mbuga zote ukitaka kwenda lazima upite Monduli na hili nitalisimamia uchumi wa Monduli kuongezeka kupitia Utalii, na nitakuwa mkali kwa hiyo ukisikia tumevutanavutana hakuna mtu wa kumuonea mwenzake lengo ni kufika mahali sahihi "amesema DC Mwenda Monduli.

Share To:

Post A Comment: