Mkuu wa wilaya ya Nachingwea Mohamed Hassan Moyo akikagua moja ya barabara inayojengwa wilayani humo
Mkuu wa wilaya ya Nachingwea Mohamed Hassan Moyo akikagua moja ya barabara inayojengwa wilayani humo
Mkuu wa wilaya ya Nachingwea Mohamed Hassan Moyo akikagua moja ya barabara inayojengwa wilayani humo

Na Fredy Mgunda, Nachingwea.

MKUU wa wilaya ya Nachingwea Mohamed Hassan Moyo amewataka TARURA kumsimamia mkandarasi anayejenga barabara ya Chimbendenga Majonanga kata ya Mbondo kujenga barabara kulingana na thamani ya fedha zilizotolewa na serikali ya awamu ya sita.


Akizungumza wakati wa ziara ya kusikiliza kero za wananchi,Moyo alisema kuwa serikali ya awamu ya sita imekuwa ikitoa fedha za miradi lakini watendaji wamekuwa hawasimamii vizuri miradi.

Moyo alisema kuwa barabara hiyo inaurefu wa kilometa 35 yenye thamani ya shilingi millioni 400 kwa ajili ya kurahisisha usafiri kwa wananchi wanaotumia barabara hiyo.

Alisema kuwa barabara hiyo inatakiwa kukamilika kwa wakati la sivyo atakuwa mkali kwa mtu yoyote atakayezichezea fedha za miradi ya maendeleo ya wananchi na serikali.

Kwa upande wake meneja wa TARURA wilaya ya Nachingwea,Enock Mshiha alisema kuwa ujenzi wa barabara hiyo umefikia asilimia 60 na mkandarasi ameshalipwa kiasi cha shilingi millioni 200 hadi sasa.

Mshiha alisema kuwa amepokea maelezo ya Mkuu wa wilaya ya Nachingwea Mohamed Hassan Moyo na atayafanyia kazi kwa kuhakikisha miradi yote ya TARURA wilayani humo inakamilika kwa wakati na ubora unaolingana na thamani ya fedha za miradi
Share To:

mwangaza wa hbari

Post A Comment: