Mkuu wa wilaya ya Iringa Veronica kessy akiyekaa katika akiwa makini kumsikiliza mwenyekiti wa chama cha mapinduzi CCM Manispaa ya Iringa Said Rubeya


Na Fredy Mgunda, Iringa.

Mkuu wa Wilaya ya Iringa amewataka watendaji wa mitaa,Kata na Tarafa kuwakamata wazazi na walezi wote ambao hawajawapeleka watoto Shule bila sababu za msingi na anataka taarifa kamili siku ya jumatatu.



Akizungumza  wakati wa Mkutano wa Wajumbe wa Kamati ya Ushauri ya Wilaya ya Iringa (DCC), mkuu wa wilaya ya Iringa Veronica Kessy alisema kuwa anataka taarifa iliyokamilika siku ya jumatatu ili kujua wanafunzi wangapi hawajaenda shule na sababu zao.


"Wanafunzi wote wa kidato cha Kwanza wanaotakiwa kwenda shule waende Mara moja Shule na taarifa niikute mezani kwani muda umepita shule zimefunguliwa tarehe 9 mwezi wa kwanza mpaka leo hivi tunazungumza ni tarehe 15 mwezi wa pili, huyu mtoto ambaye hajaripoti shule mpaka leo tunategemea tupate matokeo mazuri kweli. Kwahiyo niliagiza ufanyike Msako, wazazi na walezi ambao watoto wao hawajaenda Shule wakamatwe" alisema Kessy


Kessy alisema kuwa anaomba kujua ni wazazi wangapi ambao wamekamatwa kwa kosa la kutowapeleka watoto wao shuleni na majibu yao yalikuwa yapoje? Aliuliza mkuu wa wilaya ya Iringa.


Aliomba kupata ripoti ya Kinachoendelea kutoka kwa Afisa Elimu na kumtaka Katibu tawala wa Wilaya ya Iringa (DAS) kufanya usimamizi pamoja na Utekelezaji wa maagizo hayo. 


"Wazazi wote ambao Watoto wao hawajaenda Shule wakamatwe, kuna tabia ya Watendaji kukaa na kuwatetea wazazi, ila nashukuru Kwasababu karibia kila Kata ina Polisi kata sasa hivi, mkafanye msako makawakamate mpaka mtoto aende shule vinginevyo awe na sababu tofauti labda kifo na kama ni mimba atwambie mimba hiyo ni ya nani, kama ameozesha ndo tunaenda naye moja kwa moja mahakamani, ifanyike hivyo hivyo kwa darasa la Kwanza na Awali kwani tuliweka makadirio ili tupate mrejesho wake tujue ni asilimia ngapi" alisema Kessy


Mkuu wa wilaya ya Iringa Veronica Kessy alimaliza kwa kuwataka Viongozi kufuata Maelekezo yanayotolewa na ofisi yake na kuyafanyia kazi Mara moja.


Kwa upande wake Afisa Elimu sekondari Manispaa ya Iringa Tupe kayinga alisema kuwa wameshafanya tathimini ya kujua watoto wangapi hawaripoti shule na sababu zao na kumuahidi mkuu wa wilaya ya Iringa Veronica kessy ifikapo siku ya jumatatu watampelekea taarifa kamili.


Kayinga alimhakikishia mkuu wa wilaya ya Iringa Veronica kessy kuwa wamekuwa makini kufuatilia suala la wanafunzi kuripoti shule kwa umakini mkubwa na matokeo yake yamekuwa mazuri.


Share To:

mwangaza wa hbari

Post A Comment: