Diwani wa kata ya Ruaha Manispaa ya Iringa Tandesi Sanga akifanya usafi na wanafunzi wa chuo cha CDTI Iringa ikiwa ishara ya kuwahimiza wananchi kufanya usafi na kutunza mazingira.
Baadhi ya wanafunzi wa chuo cha CDTI Iringa wakiwa na mabango ambayo yanasisitiza wananchi kufanya usafi na kutunza mazingira
Baadhi ya wanafunzi wa chuo cha CDTI Iringa wakiwa wanafanya usafi kwenye mazingira ambayo wananchi wanaishi kwa lengo la kuikumbusha jamii kufanya usafi na kutunza mazingira yanayowazunguka.

Na Fredy Mgunda, Iringa.

CHUO cha mendeleo ya Jamii Ruaha CDTI kimeitahadharisha jamii kujiepusha na uchafuzi wa mazingira ikiwemo utupaji taka hivyo katika maeneo yao hali inayowaweka hatarini kukumbwa na magonjwa ya mlipuko yatoka na uchafu.


Makamu mkuu wa Chuo taaluma CDTI Ruaha Osward Muheni akizungumza wakati wa zoezi la hamasa ya usafi wa mazingira Kwa vitendo lililotekelezwa na Chuo hicho ameitaka jamii kuacha utamaduni wa utupaji taka katika maeneo yasiyo rasmi na badala yake Kila mmoja kuwa balozi wa usafi Kwa kukemea uchafuzi wa mazingira

Muheni alisema anachukizwa na tabia ya baadhi ya wafanyabiashara na Wananchi wengine katika maeneo mbalimbali ikiwemo Manispaa ya Iringa kufanya usafi katika maeneo yao Kisha kukusanya taka na kuzitupa barabarani ama katika maeneo katika maeneo ya wazi jambo ambalo alisema linapaswa kukemea vikali huku akiziomba mama husika ikiwemo Serikali kuchukua hatua hatua Kali Kwa watakaobainika.

"Nia aibu Kwa mtu mwenye akili timamu kufanya usafi kusafisha ndani ya duka ama nyumba yake Kisha kukusanya uchafu na kuzitupa barabarani, tena inashangaza baadhi Yao ubeba uchafu pipa la taka lakini badala ya kuiweka uchafu huo ndani ya pipa/Chombo wao utupa nje na kufanya maeneo yetu kuwa machafu wakati wote" Alisema Osward Mheni 

Makamu mkuu huyo wa Chuo Cha maendeleo ya Jamii Ruaha CDTI kilichopo Ipogolo Manispaa ya Iringa aliwataka wanajamii kutambua athari za magonjwa ya Mlipuko kuwa ni pamoja na Gharama kubwa za matibabu pindi yanapozuka magonjwa ya mlipuko ikiwemo Kipindupindu huku akiitaja athari kubwa Zaidi ni vifo vitokanavyo na maradhi yanayosababishwa na uchafu.

Aidha Kwa upande wake  Mkufunzi Chuo Cha Maendeleo Ruaha CDTI Mhidini Gariatano alisema zoezi la hamasa ya usafi wa mazingira lililotekelewa na Chuo hicho ni zoezi endelevu huku akiwataka wanachuo walioshiriki kufanya usafi katika mitaa mbalimbali ya Kata ya Ruaha manispaa ya Iringa Kuwa kutumia nafasi waliyo nayo kuendelea kuielimisha jamii umuhimubwa usafi katika mazingira Yao huku akiihimiza jamii kushirikiana na Chuo hicho katika kuendeleza usafi wa mazingira Kwa wakati wote.

Alisema malengo ya Chuo hicho ni kuhakikisha kila mwanajamii anakuwa mstari wa mbele katika kufanya usafi wa mazingira Ili kuhakikisha Manispaa ya Iringa na Wilaya Kwa ujumla inakuwa safi wakati wote ikiwa ni sehemu ya Jitihada za kupinga maradhi yatokanayo na uchafuzi wa mazingira.

Miongoni mwa wadau walioshiriki katika zoezi Hilo ni Mkurugenzi wa kampuni ya EnviBright ya mjini Iringa inayojihusisha na Usafi na uhifadhi wa mazingira Paul Myovela alitoa wito Kwa wanachuo kugeuza takakata zilizooza Kuwa fursa ya kiuchumi akiwahimiza kutumia Ubunifu walionao kuzigeuza taka hizo Kuwa mbolea Kwa ajili ya shughuli za kilimo.

Kando ya fursa hiyo Myovela ameiomba Halmashauri ya Manispaa ya Iringa kuitangaza fursa kwamakamupini ya usafi wa mazingira kuchukua tenda ya kufanya usafi katika maeneo hayo Ili kukomesha Tatizo la mlundikano wa taka uliokithiri katika maeneo mbalimbali.

Naye Diwani wa kata ya Ruaha Manispaa ya Iringa Tandesi Sanga  aliyeshiriki katika zoezi Hilo ameupongeza Uongozi wa Chuo Cha Maendeleo ya Jamii CDTI Ruaha Kwa kuonesha Kwa vitendo umuhimu wa Usafi akitoa wito Kwa Taasisi nyingine kuiga mfano huo katika kuhamasisha usafi wa mazingira.

Sanga alitoa wito Kwa wakazi wa Kata hiyo kuhakikisha wanaungana Kwa pamoja katika kukemea uchafuzi wa mazingira akisiisitiza Kuwa Ruaha bila uchafu inawezekana.

Diwani Tandesi Sanga pia ameomba Uongozi wa Chuo pamoja na Kuwa mstari wa mbele katika usafi wa Mazingira pia ameuomba kuratibu zoezi la upandaji miti katika maeneo mbalimbali kwa Lego la kuunga mkono Jitihada za Serikali ya awamu ya Sita iliyo chini ya Rais Samia Suluhu Hassan katika Uendelezaji na Uhifadhi mazingira pamoja na Usafi katika maeneo yote ya nchi.

Share To:

mwangaza wa hbari

Post A Comment: