Mjumbe Halmashauri kuu ya chama cha mapinduzi Taifa MNEC Salim Abri Asas akiongea na wananchi na wanachama wa chama cha mapinduzi CCM Mkoa wa Iringa katika kata ya kiyowela wakati wa uzinduzi wa miaka 46 ya kuzaliwa kwa chama hicho.
Mjumbe Halmashauri kuu ya chama cha mapinduzi Taifa MNEC Salim Abri Asas  akizundua ujenzi wa ofisi ya chama cha mapinduzi CCM kata ya kiyowela
Mjumbe Halmashauri kuu ya chama cha mapinduzi Taifa MNEC Salim Abri Asas  akizundua ujenzi wa ofisi ya chama cha mapinduzi CCM kata ya kiyowela
Hii ndio ofisi ya kata kiyowela iyojengwa kwa ufadhili mjumbe Halmashauri kuu ya chama cha mapinduzi Taifa MNEC Salim Abri Asas  akizundua ujenzi wa ofisi ya chama cha mapinduzi CCM kata ya kiyowela


Na Fredy Mgunda, Iringa.


MJUMBE Halmashauri kuu ya chama cha mapinduzi Taifa MNEC Salim Abri Asas amefadhili ujenzi wa ofisi ya CCM kata ya Kiyowela wilayani Mufindi, mkoani Iringa itakayogharimu zaidi ya Sh Milioni 52 pindi itakapokamilika. 

Uzinduzi wa ofisi hiyo ambayo ujenzi wake unaendelea imezinduliwa leo na MNEC huyo wakati chama hicho kikizindua maazimisho ya miaka 46 ya chama hicho.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, MNEC Salim Abri Asas alisema kuwa lengo la kujenga ofisi ofisi hiyo ya kata ya kiyowela ni kutokana kuwa na mapenzi ya kweli na chama cha mapinduzi.

Asas alisema kuwa Wananchi na wanachama wa chama cha mapinduzi kata ya kiyowela waliongoza kwa kupiga kura nyingi kwa viongozi wa chama cha mapinduzi na kuongoza kitaifa hivyo ndio maana hata maazimisho ya uzinduzi wa miaka 46 ya kuzaliwa kwa chama hicho yamefanyikia huko.

Alisema kuwa chama cha mapinduzi CCM Mkoa wa Iringa kimejipanga kuhakikisha kinajenga ofisi za chama hicho kila kata ili wananchi na wanachama wanaweza kwenda kwenye ofisi hiyo kutatuliwa kero zao kama ilivyokuwa awali.

Awali akisoma taarifa ya ujenzi wa ofisi hiyo,Katibu wa CCM kata ya Kiyowela Basil Msakwa alisema kuwa kata ya Kiyowela ina jumla ya wanachama 2000 kutoka katika matawi matatu ya chama hicho ambayo ni Magunguli, Isaula na tawi la Kiyowela.

Msakwa alisema kuwa Asas amefadhili ujenzi huo kama moja ya pongezi zake kwa kata hiyo iliyoongoza kwa kupiga kura nyingi za Rais, wabunge na madiwani katika uchaguzi wa mwaka 2020 ambapo walipiga kura kwa asilimia 100.

Msakwa alisema kuwa kata hiyo inakabiriwa na changamoto za kutokuwa na miradi hai ya kiuchumi ya ndani ya kata pamoja na tatizo la miundombini kwenye taasisi za Serikali zilizopo kata hiyo.

Alimalizia kwa kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuitekeleza ilani ya uchaguzi ya mwaka 202/2025.

Share To:

mwangaza wa hbari

Post A Comment: