Baadhi ya Wanachama wa Chama Cha Mapinduzi CCM Mkoani Arusha wamemkata na kusema hawatampigia kura Mgombea wa nafasi ya Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa NEC kuipitia Mkoa wa Arusha Gesso Bajuta nakudai kuwa ni Diwani wa Kata Endamilay wilayani Mbulu, Mkoani Manyara na hawapo tayari kumchagua mtu ambaye tayari ni Kiongozi Kwenye mkoa mwingine.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti kupitia blog hii wameeleza kusikitishwa na kitendo Cha Mgombea huyo kuchukua fomu Mkoa wa Arusha na kuacha  kuchukua fomu katika Mkoa anaouongoza katika nafasi ya udiwani.

"Sisi tunaenda kupiga kura kumchagua mtu ambaye atakisaidia Chama chetu Cha Mapinduzi na Kiongozi ambaye tukimuhitaji mudaa wowote tunampata na sio mtu anayetaka uongozi Kwa maslahi yake bianafsi"


Share To:

Post A Comment: