Angela Msimbira TAMISEMI

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe. Angellah Kairuki amewataka watumishi wote wa Wizara, Taasisi zilizopo chini ya Wizara hiyo, Sekretarieti za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa kufanyakazi kwa kuheshimiana, kuaminiana na kushirikiana ili kumsaidia Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan.

Ametoa kauli hiyo leo Oktoba 6, 2022 jijini Dodoma mara baada ya kukabidhiwa Ofisi na aliyekuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais – TAMISEMI Mhe. Innocent Bashungwa ambaye aliteuliwa kuwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa.

“Najua uwezo wa  watumishi wa Ofisi ya Rais –TAMISEMI, wanataaluma na uwezo mkubwa, hivyo tumienu utaalam wenu kunishauri na ninaamini kwa nguvu niliyoiona hapa tutafanikiwa”  amesema Waziri Kairuki 

Waziri Kairuki amewataka watumishi hao kufanyakazi kwa uwazi, weledi na kuhakikisha kazi zinakamilika kwa wakati na ubora wa maandiko ili kufikia malengo yaliyowekwa na Wizara.

“Tuwe wawazi na moyo mweupe maana mimi ni mkali ukienda ndivyo sivyo, tukamilishe kazi kwa wakati, lakini kuwepo ubora wa andiko unaloleta likiwa vibaya tutagombana na safari itaishia hapo lakini naamini kwa nguvu ninayoiona hapa tutafika mbali,”amesisitiza Waziri Kairuki.

Vilevile, amewataka watumishi hao kuacha kufanyakazi kwa mazoea na kuendekeza majungu bali amewataka kila mmoja kwa nafasi yake kutimiza majukumu yake kwa wakati na kikamilifu lengo likiwa ni kuhakikisha tunawadumia wananchi.

Awali, akizungumza kabla ya kukabidhi ofisi, Waziri Bashungwa amemhakikishia  Waziri Kairuki kuwa atakuwa sehemu ya ushirikiano huku akiwaasa watumishi hao kuendelea kufanyakazi kwa ushirikiano na  kuwa timu moja.

Naye, Naibu Waziri Tamisemi anayeshughulikia Elimu, Mhe. David Sil CGinde ameeleza katika utawala huu wa awamu ya sita hakuna kijiji ambacho hakina mradi wa serikali huku akimwahidi ushirikiano Waziri Kairuki.Share To:

Post A Comment: