Mkuu wa Mkoa wa Tanga Omary Mgumba ameagiza kusimamishwa kazi na kuhojiwa na Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (TAKUKURU) watumishi wanne  wa Halmashauri ya Muheza kutokana na matumizi mabaya ya fedha na usimamizi mbovu wa miradi ya Maendeleo.

Mkuu wa Mkoa huyo amechukua hatua hiyo wakati wa ziara yake Wilayani humo iliyokuwa na lengo la kukagua miradi ya maendeleo.

Kusimamishwa kwa watumishi hao kumekuja ikiwa ni mwezi mmoja na siku 19 kupita kwa  aliyekuwa Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo  Nassib Mbaga kusimamishwa kazi na aliyekuwa Waziri wa Tamisemi Innocent Bashungwa  Kutokana na kushindwa kusimamia majukumu yake ipasavyo na utendaji kazi usioridhisha. 

Watumishi hao waliosimamishwa ni Ramadhani Mtingi (Idara ya ujenzi), Zainabu Mzindakaya ,Muweka hazina wa Halmashauri (DT), Furaha Sarakikya Idara ya Manunuzi na   Afisa Elimu Sekondari Serapion Basgange

" Tunaanzia na hawa wa nne na wengine  kadri ninaavyopata taarifa  nitatoka maelekezo  na hawa sio wasimame kupisha uchunguzi maalum lakini pia takukuru uanze kuhangaika nao" Alisema Mgumba nakuongeza kuwa  haiwezeni waeendelee kubaki kwenye utumishi wa umma ndani ya Muheza maana hata madarasa tuliyopewa hayatakamilika na watoto hawawezi kuanza sababu wamesema milion 20  haikamilishi darasa nakwamba wanataka milion 35 Kwa darasa.

Pia ameagiza  Mkazi wa hesabu za Serikali CAG afanye ukaguzi Maalum Kwa miaka mitatu mfurulizo  katika miradi yote ya maendeleo Wilayani humo.

Share To:

emmanuel mbatilo

Post A Comment: