************* 


WASHIRIKI wa Shindano la dunia la utanashati,urembo na mitindo kutoka nchi mbalimbali wafanya utalii wa ndani kujifunza vitu vinavyopatikana nchini Tanzania. 


Akizungumza na Wanahabari Mkurugenzi idara ya sanaa dkt.Emmanuel Ishengoma amesema Kayla ya kufanyika shughuli hizo za Shindano hilo washiriki wamepata fursa ya kufanya utalii wa ndani ikiwemo kutembelea ukumbi maalum utakaofanyika Shindano hilo, daraja jipya la Tanzanite pamoja na Fukwe za bahari ya coco liyopo Jijini Dar es salaam. 


"Washiriki wetu wamepats nafasi hiyo ya kutembelea ukumbi mahsusi utakaofanya shughuli yetu ,daraja la Tanzanite na kumalizia fukwe za Bahar ya coco Beach lakini mategemeo yetu tutakwenda visiwani zanzibar na kumalizia hifadhi ya Ngorongoro." 


Mwenyekiti wa chama cha viziwi nchini ( Kisuvita) Habibu Mrope ameeleza kuwa maandalizi yamekamilika na washiriki wanaendelea na hatua za mwisho huku akiongeza kuwa Shindano la mwaka 2022 limebeba washiriki wazuri zaidi. 


" huwezi tabiri nani anaweza kuibuka mshindi kutokana maandalizi mazuri na mvuto kwa kila mshiriki anaeshiriki Shindano hilo ."
Share To:

emmanuel mbatilo

Post A Comment: