Watu wanne wamefariki dunia baada ya lori kugongana na bajaji katika eneo la Kinyanambo- Mafinga, Wilaya ya Mufindi mkoani Iringa

 Akizungumza na Mwananchi leo Jumatano Oktoba 19, 2022 Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Mji Mafinga, Dk Victor Msafiri amesema ajali hiyo ilitokea jana usiku.

Dk Msafiri amesema walipokea miili ya wanaume wawili, mwanamke mmoja na mtoto mmoja.


Amesema kuwa hadi sasa mwili mmoja tayari umeshatambuliwa na ndugu kwa ajili ya kuendelea na taratibu zingine za mazishi huku miili mingine ikiwa bado imehifadhiwa katika hospitali hiyo.

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoani Iringa, Kamishna Msaidizi wa Polisi,  Issa Juma Suleiman amesema chanzo cha ajali hiyo ni uendeshaji usiozingatia sheria za usalama barabarani.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Madereva Bajaji Mafinga Mjini, Arouni Manga amesema walipokea taarifa kwamba kuna ajili maeneo ya Kinyanambo.

"Ni kweli tulifikia hadi eneo la tukio tulikuta bajaji ikiwa imelaliwa na lori tulipojaribu kuitoa tulikuta watu wote wamepoteza maisha akiwa na dereva wetu ila kwa sasa tupo njia tunaelekea Songea kwa ajili ya kumpunzisha dereva mwenzetu katika nyumba yake ya milele" amema Manga

Pia ameeleza kuwa mji wa Mafinga umekuwa na msongamano mkubwa wa vyombo vya moto hivyo kuiomba Serikali kuangalia namna bora ya kujenga barabara za pembeni ili bajaji ziweze kupita katika njia hizo.

"Mfano nzuri kwa wenzetu wa mji wa Makambako wamejengewa barabara za pembeni ndio ambazo wanazitumia hivyo tunaiomba Serikali kutujengea barabara hizo ili kupunguza ajili na kuokoa maisha ya abira na madereva bajaji katika Mji wetu." amesema Manga

Share To:

Post A Comment: