Na John Walter-Babati Jamii katika Kijiji cha Luxmanda Kata ya Secheda Halmashauri ya wilaya ya Babati Mkoani Manyara wametakiwa kutambuwa wajibu wao katika kulinda na kusimamia haki za watoto pamoja na kuwapa fursa ya kupata elimu bora katika mazingira rafiki ya kujisomea ili kukuza taaluma na kukabiliana na ukatili wa kijinsia. Akizungumza kwa niaba ya Katibu Tawala Mkoa wa Manyara, Afisa taaluma wa Mkoani hapa Mwl.Julita Ako, wakati wa Kilele cha Juma la elimu katika shule ya Secondary Ufana amesema imebainika kuwa changomoto za kimazingira ya Baadhi ya Wanafunzi kuishi katika nyumba za kupanga (Gheto) zinapelekea Wanafunzi hao kukumbwa na matukio ya ukatili wa kijinsia na kupelekea kushuka kitaaluma. Afisa Taaluma huyo amesema "Ufaulu wa mtoto katika shule na Maendeleo ya kitaaluma haviwezi kuwepo bila ya ushirikiano wa jamii,viongozi pamoja na Wanafunzi ambapo katika jukwaa la elimu Wanafunzi wameweza kushirikiana na wazazi katika kutoa jumbe zao ikiwemo maswala ya ukatili wa kijinsia hali inayoshusha taaluma" Naye Mkuu wa Shule Secondary Ufana Mwl. Haikasia Minja amesema Wanafunzi wengi wanaoishi katika nyumba za kupanga (Gheto) wamekuwa hawafanyi vema kitaaluma kutokana na changomoto mbalimbali ya kukosa mahitaji pamoja na Malazi hali inayopekewa utoro shuleni hapo hivyo kupitia Juma la elimu wazazi na walezi wametakiwa kujenga utamaduni wa kujuwa Maendeleo ya watoto wao pamoja na changomoto zao. Mwl. Minja amesema "Juma la elimu inawakutanisha walimu na Wanafunzi pamoja na wadau wa elimu wakiwemo wazazi na walezi Huku lengo kubwa ikiwa ni kukuza taaluma na kuondoa alamaa sifuri katika matokeo ya mitiahani,kudhibiti utoro na kuwakumbusha wazazi wajibu wao katika kuwafanikishia Wanafunzi kufanya vizuri kitaaluma. Akizungumzia matukio ya ukatili wa kijinsia Mwl.Minja amesema Wanafunzi wengi wanaokaa gheto wanaporudi jioni wao ndio Baba au Mama wanaanza majukumu kama wazazi wenye familia na kuanza Kutafuta mahitaji na maandalizi ya chakula cha jioni hali inakuwa ngumu zaidi pale ambapo mzazi anapochelewesha fedha kwaajili ya kununulia chakula" Aidha Diwana wa kata ya secheda Mh. Ibrahimu Tatock pamoja na wazazi Samweli Kwangu Na Julius Majengo amesema wapo tayari kushirikiana kwa pamoja katika kuboresha mazingira ya kujifunzia pamoja na kukabiliana na ukatili wa kijinsia kwa Wanafunzi wanaoishi katika nyumba za kupanga (Gheto) ili kukuza taaluma kwa Wanafunzi pamoja na Maendeleo shuleni Hapo. Nao Baadhi ya Wanafunzi wa Shule ya Ufana secondary Michael Martin na Elisha wamesema kupitia Juma la elimu inayoadhimishwa kila Mwaka shuleni hapo imesaidia kuwaunganisha wazazi na Wanafunzi katika kutambuwa wajibu wao hasa katika kuza taaluma na Kutafuta changomoto zinazowakabili Wanafunzi shuleni hapo.
Share To:

Post A Comment: