Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara Christina Mdeme,  amefanya kikao cha ndani na Viongozi wa CCM na Jumuiya zake kutoka wilaya za Mkoa wa Arusha kwa ajili ya kuwanoa viongozi waliochaguliwa katika ngazi ya Wilaya na Kata.


Katika kikao hicho kilichofanyika jana, Naibu Katibu Mkuu amewafunda viongozi hao kuhusu mambo mbalimbali ikiwemo ikiwemo kujiepusha na Makundi, kufanya kazi ya chama kwa weledi, uendelezaji na uanzishaji wa miradi mipya huku wajiepusha na rushwa kuelekea Uchaguzi wa Mkoa.

" Ndugu Viongozi pia nasisitiza kuhakikisha mnaakuwa mstari wa mbele katika kuyasema mazuri ya Serikali ya awamu ya sita chini ya Mwenyekiti wa Chama Rais Samia Suluhu Hassan na kuwa mstari wa mbele 'kuchonga barabara' ya kutupeleka kwenye ushindi wa kishindo mwaka 2025 - 2030," akasema Naibu Katibu Mkuu.

Aidha Naibu katibu Mkuu alifanya ziara ya kukagua miradi mbalimbali ya vitegauchumi iliyopo katika Kata, wilaya na Mkoa huo wa Arusha ambapo amewapongeza viongozi wa Arusha kwa kuendelea kuwa kinara katika nyanja ya kujitegemea kwa kuwa na uchumi mkubwa.




Share To:

Post A Comment: