Mamlaka ya udhibiti mbolea Tanzania Kanda ya Kaskazini (TFRA) kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Moshi wamefanikiwa  kukamata mbolea feki za ruzuku zikiuzwa maduka ya soko la Mbuyuni.


Akizungumza katika msako huo mara baada ya kupata taarifa kutoka kwa mkulima wa Wilaya ya Siha aliyedai kuuziwa mbolea feki,Albert Mwaulambo Afisa udhibiti ubora wa huduma wa mbolea Tanzania Kanda ya Kaskazini (TFRA) amesema kuwa mbolea walioikamata haifai kwa matumizi na siyo mbolea inayozalishwa na kampuni ya YARA kamali ilivyo kuwa imehifadhiwa."Tumekagua mbolea hiyo ni vumbi tupu na tumebaini kuwa wauzaji hao wanauza mbole ya ruzuku kwa bei ya juu ya shilingi elfu tisini (90,000) badala ya elfu sabini (70,000)" alieleza Mwaulambo.


Aliongeza kusema kuwa katika maduka mawili waliyoyakagua duka moja wamebaini halina namba ya uwakala wa kuuza mbole za ruzuku huku likiuza mbolea ya Super gro isiyokuwa na usajili na muuzaji mmoja kati ya watatu akiwa ndiye mwenye mafunzo wakati duka lingine likiuza mbolea hiyo feki.


Mkuu wa Wilaya ya Moshi Abbas Kayanda akizungumza katika tukio hilo la ukamataji wa mbolea hizo feki ameeleza kuwa hatua kali za kisheria zitachukuliwa ili kukomesha unyonyaji unaofanywa na baadhi ya wauzaji wa pembejeo za kilimo wasiyo waaminifu unaosababisha wakulima kupata hasara."Tume shuhudia vumbi la mbolea feki ya ruzuku kutoka kampuni ya YARA ambapo mwananchi mmoja kutoka wilaya ya Siha aliuziwa mbolea hiyo Moshi Mjini alipo toa taarifa kwa Afisa kilimo ndipo tukafanya ukaguzi katika duka alilouziwa tukabaini mbolea nyingine zikiwa ni feki na mwenye duka amekiri kumuuzia mbolea hiyo,hatua kali za kisheria zitachukuliwa ili kukomesha tabia hiyo ya kuwanyonya wananchi katika shughuli zao za kilimo"alieleza  Kayanda .


Aliongeza kusema kuwa  tayari wamekubaliana na wataalamu wa kilimo kufanya ukaguzi katika maduka yote yanayo uza pembejeo za kilimo ili kujiridhisha na aina ya mbolea wanazo uza pamoja na bei elekezi ya serikali ili kumnusuru mkulima kupata hasara wakati serikali imetengeneza mazingira rafiki kwa wakulima.


Rais Samia Suluhu Hassan tayari alishatoa maelekezo juu ya upatikanaji wa mbolea za ruzuku ili mkulima asipate hasara ikiwa ni pamoja na kuinua sekta ya kilimo hivyo Wauzaji wote waliyowakamatwa watachukuliwa hatua za kisheria ili wengine wazidi kujifunza huku wale ambao ni wakala wa mbole ya ruzuku kutakiwa kuzingatia maelekezo ya serikali.


Awali akieleza kuhusu kuuziwa mbolea feki ya ruzuku Mkulima Caroline Martin alidai kuwa hakuwa na shaka kutokana na kuonekana imehifadhiwa vizuri ila alipo fika shambani ndipo alipo gundua ni feki.


"Mimi ni mkulima wa mboga aina ya Kabeji siyo mara ya kwanza kutumia hiyo mbolea ila kwa mara hii imenishangaza,nilipo fika shambani pamoja na vibarua wangu ndipo niligundua ni feki kwani ukiishika mkononi haina ukali wowote kama inavyopaswa kuwa".


Aliongeza kuwa " niliilamba mdomoni kusikia ladha yake siku sikia kitu zaidi ya udongo mtupu na siyo mbolea,nimepata hasara ya fedha ya kununulia, usafiri pamoja na vibarua maana nilikuwa nimesha walipa,naomba serikali iangalie hili jambo wakulima wanapata hasara na hawasemi" alieleza.

Share To:

Post A Comment: