Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi, Richard Rwehumbiza,  akifungua kikao cha tathmini na uzinduzi wa mradi wa kutokomeza ukatili wa kijinsia, ikiwemo ukeketaji, na mila potofu mbele ya Kamati ya MTAKUWWA ngazi ya Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi kupitia ufadhili wa Shirika la Foundation Civil Society (FCS). Kutoka kushoto ni  Mkurugenzi wa ESTL Joshua Ntandu Lisu na kulia ni Afisa Maendeleo ya Jamii wa wilaya hiyo, Mariam Mwandikile ambaye alikuwa Mwenyekiti wa kikao hicho.  

 Mkurugenzi wa ESTL Joshua Ntandu  Lisu, akitoa taarifa ya mradi waliofanya kwa kipindi cha miaka minne katika Halmashauri ya Wilaya ya Singida DC na Singida Manispaa. Katikati ni Afisa Elimu Msingi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi, Margaret Kapolesya .
Afisa Maendeleo ya Jamii Wilaya ya Ikungi, Mariam Mwandikile akichangia jambo kwenye kikao hicho.
Mganga wa Shirika la ESTL, Getrude Liberatus akizungumzia mbinu mpya zinazotumika kuwafanyia ukatili wa kijinsia watoto.
 Mkaguzi wa Uhamiaji Wilaya ya Ikungi Abel Shindayi  akichangia jambo kwenye kikao hicho.
Mkuu wa Polisi Wilaya ya Ikungi (OCD) Suzana Kidiku (kulia) na  Mkaguzi wa Uhamiaji Wilaya ya Ikungi Abel Shindayi wakiwa kwenye kikao hicho.

 Afisa Mawasiliano na Vijana wa shirika hilo Edna Mtui (kushoto) akiteta jambo na Ofisa wa shirika hilo, Aisha Msuya.

Afisa Elimu Msingi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi, Margaret Kapolesya .akisisitiza jambo kwenye kikao hicho.
Kikao kikiendelea.
Kikao kikiendelea.
Wadau wakiwa kwenye kikao hicho.

Muhudumu wa Afya Ngazi ya Jamii wa shirika hilo, Hawa Njolo akichangia jambo kwenye kikao hicho.
Afisa Miradi wa Shirika hilo, John Nzungu akielezea utekelezaji wa mradi huo wilayani Ikungi.
Sheikh wa Kata ya Ikungi, Salum Ngaa akichangia jambo kwenye kikao hicho.
Mchungaji wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Wilaya ya Ikungi, Joyce Madadi akizungumza kwenye kikao hicho.
Mwanasheria wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Ombeni Komba akichangia jambo kwenye kikao hicho.
Msimamizi wa Miradi wa shirika hilo, Chrian Zimbaiya akichangia jambo kwenye kikao hicho.
Taswira ya kikao hicho.
Picha ya pamoja.
Wafanyakaziwa ESTL wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kikao hicho. 

 Na Dotto Mwaibale,Singida. 

SHIRIKA la Empower Society Transform Lives (ESTL) linalojihusisha na masuala ya kupinga ukatili wa kijinsia  limezindua rasmi huduma za elimu na uwezeshaji jamii kwenye wilaya ya Ikungi mkoani hapa ambazo pamoja na mambo mengine zitajikita katika kuhakikisha elimu ya kutosha inatolewa kwa wana Ikungi hususani kwenye kata mbili za Kikio na Misughaa katika muktadha wa dhana hasi ya kuondokana na vitendo vya ukatili kwa wanawake na watoto.

Kabla ya huduma hizo kutolewa wilayani Ikungi shirika hilo lisilo la kiserikali kwa udhamini wa Ubalozi wa Finland,Uholanzi na Shirika la Foundation Civil Society (FCS)  katika kipindi cha miaka minne (2018/2022 limefanikiwa kuzifikia takribani kata 28 ndani ya Wilaya za Singida Manispaa na Singida Vijijini kwa utekelezajiwa huduma kama hizo.

Kwa mujibu wa shirika hilo huduma nyingine walizofanikiwa kuzitoa kwenye maeneo hayo ni pamoja na uanzishwaji wa utaratibu wa utoaji huduma mbalimbali ndani ya eneo moja (One Stop Centre), uundaji wa kamati za MTAKUWWA zipatazo 39 sambamba na uanzishaji wa mfumo maalumu wa TEHAMA ambao umekuwa ukifanya kazi ya kufuatilia kesi za matukio ya ukatili-ambapo kwasasa shirika lina mpango wa kuuwezesha mfumo huo kufanya kitaifa.

Akizungumza wakati akifungua kikao cha tathmini na uzinduzi wa mradi huo, mbele ya kamati ya MTAKUWWA ngazi ya halmashauri ya wilaya ya Ikungi kupitia ufadhili wa Shirika la Foundation Civil Society (FCS) , Mkurugenzi wa ESTL Joshua Ntandu Lisu alisema wilaya hiyo ina vihatarishi vikubwa vya matukio ya ukatili kwa wanawake na watoto kutokana na jiografia yake ya mipaka na wilaya za jamii ya wafugaji za Hanang (Manyara) na Kondoa (Dodoma) zilizopo kwenye bonde la ufa ambazo kwa kiwango kikubwa zimegubikwa na matukio ya ukeketaji.

Hata hivyo, mjumbe wa kamati ya mtakuwwa ambaye ni Mkuu wa Polisi Wilaya ya Ikungi (OCD) Suzana Kidiku alisema jeshi hilo limekuwa kwenye harakati mbalimbali za kukabiliana na matukio ya ukatili wa kijinsia kwa nyakati tofauti, ambapo kwa kipindi cha mwezi Julai hadi Septemba mwaka huu limefanikiwa kunusuru kwa kuwarejesha shuleni wanafunzi watatu ambao walikuwa hatarini kukatisha masomo yao kutokana na matukio ya ukatili.

Pia Kidiku alisema jeshi hilo wilayani hapa katika kipindi hicho limefanikiwa kufikisha kesi tatu za matukio ya ukatili wa kijinsia kwenye vyombo vya sheria, ambapo hata hivyo, mahakama iliwakuta watuhumiwa wakiwa na hatia, na wawili walihukumiwa vifungo vya hadi miaka 30 huku mmoja akiadhibiwa kifungo cha maisha.

Aidha, Mkaguzi wa Uhamiaji Wilaya ya Ikungi Abel Shindayi alisema kuna haja ya mamlaka za elimu kufanya marekebisho ya mfumo wa mtaala wa elimu uliopo kwa kuongeza kipengele cha somo la ukatili wa kijinsia, athari zake na namna bora ya kukabiliana na matukio hayo kuanzia ngazi za shule za msingi hadi vyuo ili kuwafanya wanafunzi kuwa na uelewa mpana wa masuala hayo.

Awali, akifungua kikao cha tathmini na uzinduzi wa mradi huo Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi, Richard Rwehumbiza aliwasihi viongozi wa shirika hilo kutofanya kazi kwenye kata mbili pekee bali wasambae kwenye kata zote ili kusaidia kuelimisha jamii hiyo kuachana na unyanyasaji wa aina zote hasa ukeketaji-ambao kwa sasa umeanza kuathiri hadi watoto wenye umri wa chini ya siku saba.

Share To:

dotto mwaibale

Post A Comment: