Na John Mapepele

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe, Mohamed Mchengerwa amesema  Serikali itaendelea kuwekeza kwenye timu zinazofanya vizuri huku akiwataka Watendaji wa michezo kufanya tathmini kwa zisizofanya  vizuri ili Serikali ichukue maamuzi magumu.

Mhe. Mchengerwa ameyasema haya usiku wa leo hafla ya utoaji wa tuzo kwa washindi wa mashindano  ya Afrika ya Gofu ya Wanawake -All Africa Competition Trophy (AACT) yaliyofanyika kuanzia  Septemba, 6-8, 2022 kwenye viwanja vya Gymkhana jijini Dar es Salaam na kushirisha nchi 20.


Katika mashindano hayo Tanzania imeshika nafasi ya tatu wakati Morocco imeshika nafasi ya pili na nchi ya  Afrika Kusini kuwa mshindi wa kwanza.

Ameipongeza timu ya Tanzania kwa kushika  nafasi ya tatu huku akifafanua kuwa  hayo ni matunda ya uwekezaji mkubwa wa Rais Samia Suluhu Hassan kwenye michezo katika kipindi kifupi cha uongozi wake.

Aidha, ameipongeza timu ya taifa ya soka ya wanawake ya Twiga Stars kwa kuingia nusu fainali katika mashindano ya COSAFA.

Ametoa rai kwa timu nyingine kufanya vizuri ili kuendelea kuitangaza Tanzania Kimataifa ambapo pia ametoa wito kwa wadau wengine  nchini kuendelea  kudhamini ili kukuza vipaji vya michezo.

 Hafla hiyo ilihudhuriwa na wageni mbalimbali na wadau wa michezo  ikiwa ni pamoja na Balozi wa Morocco nchini Zakaria El Goumiri na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, S

Share To:

TANGA RAHA BLOG

Post A Comment: