Daktari bingwa wa magonjwa na afya ya watoto kutoka Hospitali ya Benjamin William Mkapa Dkt Rehema Yona akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dodoma 
Mkurugenzi mtendaji Hospitali ya Benjamin William Mkapa Dkt Alphonce Chandika akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) jijini Dodoma.

 Na Janeth Raphael

HOSPITALI ya Benjamin William Mkapa imewafanyia uchunguzi wa matatizo mbalimbali ya moyo watoto 68 na asilimia 91 wamekutwa na matatizo ya moyo ya kuzaliwa nayo ikiwepo matundu kwenye moyo, matatizo kwenye mishipa ya moyo na matatizo kwenye njia ya moyo.

Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi mtendaji Hospitali ya Benjamin William Mkapa Dkt Alphonce Chandika akizungumza na waandishi wa habari leo tarehe 29 September, 2022 jijini Dodoma ikiwa ni kilele cha siku ya moyo Duniani.

Dkt Chandika amesema wao kama Hospitali ya Benjamin William Mkapa kwa kushirikiana na madakitari bingwa na wabobezi wa moyo kutoka shirika lisilo la kiserikali la One New Heart Foundation kutoka Marekani pamoja na madakitari wengine kutoka hospitali ya Rufaa bugando wameona katika kuadhimisha siku ya moyo Duniani washirikiane kwa siku tano kufanya uchunguzi na kutibu watoto wenye matatizo hayo ya moyo.

"Tuliona tuadhimishe siku hii ya leo kwa kuwahudumia watoto wa Tanzania wenye matatizo ya moyo kwa kuzingatia kauli mbiu ya mwaka huu 'TUMIA MOYO KWA KILA MOYO' tuliona tutekeleze kauli mbiu hii kwa kutumia mioyo yetu kuhudumia mioyo ya watoto wenye matatizo ya moyo na huduma hii tunaitoa bure bila malipo Kwa maana Serikali na hawa wadau kwa kishirikiana ndiyo tunagharamia matibabu ya hawa watoto" - Dkt Chandika.

Hospitali hiyo ya Benjamin William Mkapa ilianza kutoa huduma hiyo tangu tarehe 26 na watoto 68 kutoka mikoa mbalimbali nchini wamefanyiwa uchunguzi na watoto 62 wamebainika kuwa na matatizo ya moyo yanayohitaji matibabu.

"Takwimu hizi zinaweza kuwashitua ni kweli ugonjwa ni mkubwa lakini Watoto hawa 68 walibainika kuwa na dalili za magonjwa hayo kutoka hospitali mbalimbali zinazotuzunguka huko walikotoka madakitari waliwaona na kubaini kuwa wana magonjwa ya moyo na baada ya kufika hapa Benjamin hospitali baada ya uchunguzi unaona asilimia 91 wote wamebainika kuwa na matatizo ya moyo, kwa mana hiyo haya matatizo yapo na ni mengi" - Dkt Chandika.

Aidha Dkt Chandika amesema watoto hao 62 waliobainika kuwa na matatizo ya moyo wanahitaji kupatiwa huduma aidha kwa kupatiwa dawa, kufanyiwa upasuaji wa kufungua kifua au upasuaji usiohusisha kufungua kifua.

Hata hivyo Dkt Chandika amesema hospitali hiyo ina mpango wa kujenga jengo maalumu la kutolea huduma au matibabu ya moyo.

Kwa upande wake Dakitari bingwa wa magonjwa na afya ya watoto kutoka hospitali ya Benjamin Mkapa Dkt Rehema Yona amesema magonwa ya moyo kwa watoto yapo na kwa hali ya sasa magonjwa hayo yanaonekana kuongezeka.

" Watoto ni wengi wanaonekana na matatizo haya ya moyo na chanzo kikubwa cha watoto hawa kuzaliwa na magnjwa haya sababu bado haijulikani lakini zipo sababu anbazo zinapelekea vichochezi ya hawa watoto kuwa na magonjwa ya moyo ni vina saba anbavyo kuna baadhi ya watoto wamezaliwa navyo na ukichanganya na mazingira yetu kama kutumia mionzi madawa akina mama wakiwa wajawazito yanaoelekea zaidi hawa watoto kupata magonjwa ya moyo" - Dkt Rehema.

Dkt. Rehema Yona amewashauri wazazi kuwa watoto wanapougua wapelekwe mapema hospitalini kwa ajili ya uchunguzi zaidi ili wanapobainika kuwa na ugonjwa huo waweze kupatiwa matibabu haraka.
Share To:

Post A Comment: