Meneja Uhaulishaji wa Teknolojia, Biashara na Uhusiano wa Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI), Margaret Mchomvu kutoka makao makuu ya TARI Dodoma akizungumza wakati wa ufunguzi wa kongamano la msimu wa kilimo 2022/2023 wilayani Iramba mkoani Singida lililofanyika Septemba 28, 2022.
Mtafiti wa kilimo kutoka kituo cha TARI, Tumbi Tabora, Moses Adamu alielezea teknolojia ya kilimo msitu pamoja na uendelezaji wa mbegu bora.
Mtafiti wa kilimo kutoka kituo cha TARI, Tumbi Tabora, Moses Adam akizungumza na wananchi waliotembele bandala TARI wakati wa ufunguzi wa kongamano hilo. 
Mtafiti wa kilimo Ramadhani Mlawa (kushoto) kutoka Kituo cha Ilonga Morogoro akizungumza na wananchi waliotembele bandala TARI wakati wa ufunguzi wa kongamano hilo. 


Dotto Mwaibale na Philemon Mazalla, Singida


TAASISI ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI) imepeleka teknolojia ya kilimo cha mazao mchanganyiko wilayani Iramba mkoani Singida ili wakulima waweze kunufaika na kilimo.

Hayo yameelezwa na Meneja Uhaulishaji wa Teknolojia, Biashara na Uhusiano wa taasisi hiyo, Margaret Mchomvu kutoka makao makuu ya TARI Dodoma wakati akizungumza na waandishi wa habari wakati wa ufunguzi wa kongamano la msimu wa kilimo 2022/2023 wilayani humo lililofanyika Septemba 28, 2022.

Alitaja bidhaa zilizotokana na teknolojia hiyo zilizooneshwa katika kongamano hilo kuwa ni za mazao aina mbalimbali jamii ya nafaka kama mtama, mahindi, uwele,ulezi na mazao aina ya mikunde ambayo yanastawi kwa wingi mkoani Singida hasa wilayani Iramba.

Mchomvu alisema  mazao hayo ni aina ya mbaazi,mikunde, kunde zenyewe, choroko na mbaazi za muda mrefu na muda mfupi, korosho, miche, mahindi aina ya Uchavuzi Huru (OPV) na chotara ambayo wakulima wanaweza kuyanunua na mbegu za miti aina Lukina kwa ajili ya kuweza kuwaelimisha wakulima waweze kuzichagua kabla ya msimu.

“Tumewaeleza wakulima kanuni ya kilimo bora ili wajue umbali wa mche na mche na umbali kati ya mstari na mstari na namna ya kupanda kwa utaratibu huo” alisema Mchomvu.

Alisema dhumuni la TARI ni kuona mkulima analima kilimo chenye tija na bila ya kufanya kilimo hicho hata weza kuona faida ya kilimo na kushindwa kufikia mkakati wa Serikali wa ajenda 10/30 kama wataendelea kulima kilimocha mazoea.

Mtafiti wa kilimo kutoka kituo cha TARI, Tumbi Tabora, Moses Adam alielezea teknolojia za Kilimo Misitu pamoja na uendelezaji wa mbegu bora ambazo zinakingiza na wadudu, magonjwa huku zikihimili ukame na zenye tija..

Kwa upande wake Mtafiti wa kilimo Ramadhani Mlawa kutoka Kituo cha Ilonga alipata fursa ya kuzungumzia mazao ya aina tofautitofauti  ambayo wanayashughulikia zikiwemo mbegu za alizeti, kunde mbaazi na nyingine nyingi ambazo zinatija na zinaweza kuhimiri changamoto mbalimbali ya magojwa, ukame na baadhiya wadudu ambao wanashambulia mazao.

Mlawa alitaja teknolojia zingine walizozionesha katika kongamanohilo ni zile zinazotokana na mbegu zao kama vile unga wa mazao ya mihogo, mtama, viazi na viazi vitamu ambao umechanganywa na choroko. 

Alitaja vitu vingine kuwa ni biskuti, tambi, soya,bisi na mafuta ya alizeti na kuwa wanaonesha vitu hivyo ili kuonesha mnyororo wa thamani ikiwa ni kukamilisha ajenda ya Serikali ya 10/30 ambayo inasemakilimo ni biashara. 

Share To:

dottomwaibale

Post A Comment: