Kamati ya kudumu ya bunge ya huduma na maendeleo ya jamii imeridhishwa na ujenzi wa  mradi wa chuo cha ufundi Arusha (ATC) huku wakiagiza chuo hicho kuanza kutumia jengo la ufundi Tower linalogharimu takribani linalogharimu takribani sh. bilioni 2.2 pindi chuo kitakapofunguliwa ili kupunguza adha ya  mrundikano wa wanafunzi katika madarasa na maabara.

Jengo hilo la ghorofa nne limejumuisha madarasa nane yenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 880 kwa wakati mmoja,maabara sita zenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 270 pamoja na ofisi 26 zenye uwezo wa kuchukua watumishi 104.

Akizungumza   katika ziara ya kukagua jengo hilo Mwenyekiti wa kamati hiyo Stanslaus Nyongo ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Maswa mashariki amesema kuwa wameridhishwa na  jengo hilo ambapo limefikia hatua ya  kuweka samani ni vyema wakahakikisha linakamilika ili wanafunzi watakapofungua waanze kulitumia.

“Tumeshuhudia ujenzi huu upo katika hatua ya umaliziaji na kujulikana kama ufundi tower ambapo linajumuisha madarasa,maabara na ofisi za wafanyakazi kwani changamito ya madarasa katika chuo hiki ilikuwa ni kubwa na sasa imepata ufumbuzi,”amesema Mwenyekiti .
Kwa upande wake Naibu Katibu mkuu wa Wizara ya elimu sayansi na teknolojia Profesa James Mdoe amesema kuwa  chuo cha ATC kilipatiwa kiasi sh. bilioni 1.7 kutoka serikalini kupitia fedha za UVIKO-19 kwa ajili ya umaliziaji wa jengo la madarasa, maabara na ofisi lililokuwa limefikia asilimia 58.4 ya utekelezaji wake.

Aidha amefafanua kuwa mpaka sasa jengo hilo limefikia asilimia 99 ambapo fefha zilizotumika ni bilioni 1.69 huku wizara ikiwa imetoa sh. milioni 481 kwaajili ya uwekaji wa thamani na unatarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwezi huu wa septemba,2022.

“Kwa ujumla litakapo kamilika itakuwa na uwezo wa kuhudumia wanafunzi 1025 na kuweza kupunguza msongamano wa wanafunzi na watumishi katika madarasa na ofisi lakini pia kupunguza mrundikano wa ratiba za masomo kutokana na uchache wa madarasa na maabara,”amesema Prof.Mdoe.Share To:

Post A Comment: