Kuna baadhi ya watu wamekuwa wakipuuza sana ulaji wa matunda, licha ya kwamba ulaji wa matunda ni muhimu sana kwa afya zetu kwani hutusaidia sana kutukinga dhidi ya magonjwa mbalimbali.

Moja ya kazi nzuri ya matunda mwilini ni pamoja na kuifanya ngozi kuonekana vizuri pamoja na kuupatia mwili virutubisho vyote muhimu.

Zifuatazo ni baadhi ya sababu ambazo zitakufanya uendelee kupenda kula matunda na kama hupendi kula matunda basi zitakufanya uanze kula matunda.

Ndizi
Tunda hili nalo ni muhimu sana kwa afya zetu lakini pia husaidia sana kuimarisha afya ya ngozi hasa kwa wale wenye ngozi kavu.

Aidha ndizi huimarisha na kuboresha afya ya umeng'enyaji wa chakula tumboni na hivyo kumfanya mhusika kuepuka tatizo la kukosa choo.

Papai.
Ni moja ya tunda ambalo huwekwa kwenye kundi la matunda baridi, lakini pia tunda hili linafahamika sana kwa kutoa msaada kwa wale wenye shida ya kupata choo kutokana na tunda hili kuwa na uwezo mzuri wa kurekebisha mfumo wa mmeng'enyo wa chakula mwilini.

Lakini ikiwa unahitaji kulitumia tunda hili kwa kutibu ngozi yako unachotakiwa kufanya ni kuchukua tunda hili na kuchanganya na asali kidogo kisha paka usoni na ukae na mchanganyiko huo kwa dakika 10 kisha nawa fanya hivyo mara moja kila siku kwa wiki kadhaa na utaanza kuona mabadiliko.

Chungwa
Tunda hili linaingia kwenye list ya matunda makali ambayo nayo ni muhimu pia kwa afya zetu hususani afya ya ngozi kwani huwa linauwezo wa kurekebisha ngozi iliyopata majeraha kadhaa.

Umaweza kuandaa juisi yake kisha paka usoni na ukae nayo kwa masaa kadhaa bila shaka utaanza kuona mabadiliko baada ya siku kadhaa ukiwa unafanya zoezi hilo kila siku.
Share To:

Post A Comment: