**************************

----Aipongeza Wizara ya Utamaduni kwa ubunifu wa Tamasha la SENSABIKA

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa amewataka makarani wa Sensa kuwa wazalendo na kutumia lugha ya staha wanapotekeleza majukumu yao ili kupata takwimu zitakazosaidia katika maendeleo ya taifa letu.

Mhe. Majaliwa ametoa wito huo usiku huu wa Agosti 21, 2022 kwenye Tamasha la Sensabika viwanja vya Leaders jijini Dar.

Katika ujumbe wake maalum uliorekodiwa amesema Mheshimiwa Majaliwa ameipongeza wizara ya Utamaduni Sanaa na Michezo kwa kubuni kampeni maalum ya kutumia Sanaa na Michezo ya Sensabika kuhamasisha wananchi kuhesabiwa.

Amesema kuwa sensa awamu ya sita ina upekee mkubwa ukilinganishwa na sensa zote zilizopita.

Ametaja tofauti hizo kuwa ni pamoja na kuhesabiwa watu na makazi, kutumia mfumo wa TEHAMA na namna wananchi walivyo hamasika.

Aidha ametoa wito kwa wananchi kutoa ushirikiano wa kutoa taarifa zote zinazohitajika.
Share To:

emmanuel mbatilo

Post A Comment: