NAIBU waziri wa maji Mhandisi Maryprica Mahundi ameungana na watanzania kushiriki zoezi sensa ya watu na makazi huku akimpongeza Rais Samia Suluhu Hassa kwa kukuabali lifanyike licha ya kugharimu mabilioni ya fedha.


Akizungumza nyumbani kwake eneo la Iwambi Jiji Mbeya mara baada ya kuhesabiwa Mhandisi Mahundi amesema Uamuzi wa Rais Samia wa kukubali sensa na makazi lifanyike ni jambo la kupongezwa na kuungwa mkono kwani linagharimu pesa nyingi lakini kwa kutambua umuhimu wake aliridhia kufanyika."Pongezi kwa Mh Rais kwa kukubali zoezi hili kwani limegharimu pesa nyingi mfano mafunzo kwa makalani na vitendea  kazi mfano vishikwambi lakini kakubali kwa lengo kupata taarifa sahihi za wananchi kuleta ustawi katika jamii" alisema Mhandisi MahundiAkizungumzia umuhimu wa Sensa katika sekta ya Maji Mahundi alisema mara kadhaa serikali imekuwa ikitelekeza miradi lakini bado kumekuwa kukiibuka malalamiko ya kutotosheleza ni kutokana na kutumia takwimu za nyumba huku idadi ikiwa imeongezeka katika eneo husika hivyo wanaamini baada ya kumaliza kwa zoezi hili malalamiko yatakwenda kupungua kwani Serikali itakuwa inatekeleza miradi kwa usahihi na itakuwa na idadi kamili ya watu katika maeno wanayoishi kuliko ilivyo hivi sasa midari inafanywa kuwa kukadilia."Mimi kama naibu waziri wa maji Nimeungana na watanzania wote katika suala la kuhesabiwa kwani katika familia yangu usiku wa leo tumeamka watu kumi na tumetoa ushirikiano kwa marakabi na nimeshuriki sababu Sensa kwangu ni muhimu kwani mara kadhaa tumekuwa tukitekeleza miradi ya maji lakini baada ya muda huduma inaanza kutolewa unakuta  kuna malalamiko kwamba maji hayatoshi hi yote inatokana na kutokuwa na taarifa sahihi ya eneo hilo lakini tukisha jua idadi tutafanya kulingana na mahitaji" alisema Mhandisi Mary Prisca Mahundi.Aidha matika hatua nyingine Mhandisi Mahundi aliwataka watanzania kukitokeza kwa wingi kuungana na watanzani wote kushiriki zoezi la sensa ili kuiwezesha serikali kutoa huduma stahiki kwa wananchi ikiwemo afya,elimu na mahitaji mengine ya kijamii.Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Juma Homela akizungumza wakati akizindua zeozi hilo Usiku Kuamkia Agost 23 aliwataka wananchi wa mkoa wa Mbeya kujitokeza kwa ajili ya kusehabu na kutoa ushirikiano ikiwa ni pamoja na  kutoa taarifa zilizo sahihi kwa makalani wa sensa watakao pita katika maeno yao."Niwasii wanambeya wote wajitokeze kwa wingi kushiriki zoezi la sensa ili  serikali iweze kupanga bajeti yake ya kuwahudumia wananchi kwa usahihi kulingana na mahitaji" alisema Homela

Share To:

Post A Comment: