Wazir wa Maliasili na Utalii Dkt. Hazara Pindi Chana akiongea na wanahabari Jijini Arusha Mapema Leo mara baada ya kufungua Mkutano wa nane wa kimataifa wa Wanasayansi wa Mambo kale Uliondaliwa na Jumuiya ya Watafiti na Wataalamu wa Mambo kale Afrika mashariki (EAAPP) 
Mhadhiri wa chuo Kikuu Cha Marekani Prof. Jackson Njau akiongea kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi kufungua Mkutano wa nane wa kimataifa wa watafiti wa Malikale Mapema Leo Jijini Arusha


Na Ahmed mahmoud 


Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Pindi Chana Amesema kwamba Serikali itaendelea kuwapa nguvu watafiti wa Masalia ya Malikale kuandika kumbukumbu muhimu na taarifa za kweli kuhusu chimbuko la Maendeleo ya mwanadamu ikiwemo Olduvai na kwengineko ambayo itasaidia kuongeza vivutio vya Utalii na kuongeza mapato ya Taifa.


DKT. Chana Ameyasema hayo Mapema Leo wakati akifungua Mkutano wa nane wa kimataifa wa Wanasayansi wa Mambo kale Uliondaliwa na Jumuiya ya Watafiti na Wataalamu wa Mambo kale Afrika mashariki (EAAPP) unaofanyika kwa siku nne Jijini Arusha.

Amesema kwamba ndio maana serikali imeomba kupitia Wizara yake Bajeti ya Takribani bilion 620 ambayo imepitishwa na bunge ikiwa ni sehemu ya fedha hizi kuelekezwa kwtikw Utafiti wa Palcontolojia na Akiolojia kwa Lengo la kutunza historia ya Malikale na mkakati wa kutunza maeneo yetu ikiwa ni sehemu ya Historia kuhifadhi na Utafiti. 

"Leo hii utaona umuhimu wa kutangaza vivutio vyetu kulikofanywa na Rais wetu Samia Suluhu Hassan kupitia filamu ya Royal tour Sasa niwaombe wataalamu hawa kutoka mataifa mbalimbali kuja na Majibu yatakayosaidia kuona namna nzuri ya kuhifadhi nyayo ya mwadamu wa kale kule Laitol ili kuweza kuweka wigo mpana kwa Watalii wanaoitembele nchi yetu"

Awali akitoa Taarifa ya Mkutano huo Kwa Waziri Chana Jackson Njau kutoka chuo Kikuu Indiana Cha nchini Marekani amesema Mkutano huo unajumla ya washiriki 100 na Jumuiya hiyo ilianzishwa Mwaka 2007 na Wanasayansi wenye asili ya Afrika kwa Lengo la kuwaleta pamoja Waalimu watafiti wahifadhi wanafunzi wasimamizi na watunga Sera katika taaluma za Akiolojia Paleontolojia na jiolojia hususani katika bonde la ufa.

Amesema wote hao wanakutana ili waweze kujumuika kwa pamoja kubadilishana mawazo juu ya matokeo ya tafiti zao mbalimbali zinazofanyika katika bonde la ufa ambalo ndio chimbuko kuu la mwanadam Duniani kwa kawaida mkutano huo hufanyika mara 1 kila baada ya miaka 2 na Mwaka huu unawashiriki kutoka mataifa 15 Ulaya na Afrika.

Kwa Upande wake mmoja ya Mtafiti wa Malikale nchini Dkt.Charles Saanane ameomba kuwepo kwa utaratibu wa jinsi kuhifadhi Masalia ya Malikale ya nyayo za Laitol ili kuzihifadhi maana kuhamisha zitaharibika kupitia tafiti hizo za nyayo ambazo kwa Sasa zimefukiwa wapo katika Utafiti kuona namna nzuri ya kuzihifadhi kwa kujenga makumbusho kwani haiwezekani kuzihamisha baada ya Utafiti wa Awali haziwezi kuhamishika ndio maana zimehifadhiwa hapo hapo 

Amesema kupitia mkutano huo watajadili pamoja kuja na majwabu ya kuzihifadhi kwa mtindo gani awali tulifanya Utafiti wetu ili kuzibeba nw kuzihamisha tukatumia Masalia ya mnyama tukaona haiwezekani kuhamishika zinatakiwa kuhifadhiwa palepale kwani hazitakiwi kubebwa hivyo ipo haja ya kujenga makumbusho pale.

Hatahivyo Mhadhiri wa chuo Kikuu cha Dar es Saalam Dkt.Emanuel Kessy amesema kwamba chuo Kikuu Cha Dar es Salaam kimegundua nyayo za binadamu wa kale tofauti na nyayo za awali zilizogunduliwa na Dkt Merry Leaky

Alisema ugunduzi huo utasaidia kuwaleta wataalamu pamoja kuweza kuongeza kasi ya Namna bora ya kuziweka wazi nyayo hizo ilikuvutia mapato ya Taifa sanjari na namna bora ya kuzihifadhi.

Hatahivyo wageni hao wanatarajia tarehe Tano ya mwezi huu kutembelea vivutio vya Utalii katika Mji Mkongwe visiwani Unguja kabla ya kuondoka kurudi makwao
Share To:

Arusha Newsroom

Post A Comment: