CHANZO cha maji cha bonde la Milaweni,kilichopo kijiji cha Mngere,kata ya Makuyuni wilayani Monduli kitanufaisha wananchi 22448 wa Vijiji 6 ambavyo kabla walikuwa wakitembea umbali mrefu kupata maji ya kunywa na kunywesha mifugo.

Hayo yameelezwa na mkurugenzi wa rasilimali za maji, George Lugemela mbele ya waziri wa maji Jumaa Awesso, kwenye hafla ya uzinduzi wa chanzo hicho cha maji cha Milaweni,ambapo mradi huo umetekelezwa kwa fefha za mfuko wa taifa wa maji

Waziri wa maji Jumaa Awesso amewahakikishia wananchi wilayani humo kuwa vijiji vyote zikiwemo shule mbili mpya za sekondari za Mswakini na Meserani , vitapata maji ya kutosha kwa kuwa rais,ameshatoa fedha za mradi mkubwa wa maji ambao unatekelezwa na mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira jiji la Arusha AUWSA.

Amewataka watendaji wa mabonde ya maji makubwa na madogo kutokukaa ofisini na kuandaa taarifa kupitia komputa badala yake watoke watembelee vyanzo vya maji na kuhakikishaha  hakuna uvamizi unaofanywa na kuwepo shughuli za kibinadamu ambazo zinasababisha upungufu wa maji

Awali mkuu wa wilaya 
ya Monduli,Frank Mwsisumbe,amesema wilaya hiyo ina upungufu wa asilimia 32% ya maji vikiwemo Vijiji 15 na sekondari mbili mpya za Mswakini na Meserani hivyo akaiomba wizara kuipatia maji kutoka kwenye mradi mkubwa wa maji uliopo Ngaramtoni halmashauri ya Arusha DC,unaotekelezwa jijini Arusha na  mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira AUWSA,















Share To:

Post A Comment: