Asila Twaha – Mbeya

Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa imeshiriki Maonesho ya Wakulima Nane Nane Kitaifa yanayofanyika Mbeya.

TAMISEMI imeshiriki maonesho hayo ikiwa pamoja na taasisi zake zote ikiwemo TARURA, DART, Chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo, Shirika la Elimu Kibaha, Tume ya Utumishi wa Walimu , Bodi ya Mikopo ya Serikali za Mitaa na Shirika la Masoko Kariakoo.

Maonesho hayo yakiwa yamebebwa na kauli mbiu ya agenda 10/30 Kilimo ni Biashara, Shiriki Kuhesabiwa kwa Mipango Bora ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi.

Maonesho hayo yamefunguliwa leo na Mhe. Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango

Share To:

JUSLINE

Post A Comment: