Mkuu wa wilaya ya Ikungi Mhe. Jerry C. Muro leo tarehe 02/08/2022 ameweka jiwe la msingi mradi wa maji ya bomba wa rafiki ikungi utakaohudumia kata mbili za unyahati na ikungi wenye thamani ya Milioni 548  ikiwa ni sehemu ya fedha za uviko -19 


Dc Muro amesema mradi huo katika awamu ya kwanza utakuwa na maeneo nane ya umma ya kuchotea maji (vilula) na pia mradi umetengenezwa ukiwa na uwezo wa kutoa huduma ya kuwaunganisha wananchi maji majumba kutokana na miundombinu yake kupita kwenye maeneo ya makazi ya watu 


Dc Muro amesema fedha hizo ni sehemu ya fedha ambazo Mheshimiwa Rais. Samia Suluhu Hassan alizitoa kwa wilaya ya Ikungi ikiwa ni sehemu ya mapambano ya changamoto ya ugonjwa wa Uviko -19 na kwa sasa mradi umekamilika kwa asilimia 98 na vilula vyote vinatoa maji hatua itakayopungua kero ya maji katika tarafa ya ikungi


Dc Muro amemshukuru Mheshimiwa Rais. Samia kwa kuridhia ikungi kupewa fedha hizo na kumuhakikisha fedha zilizotolewa zote zimesimamiwa kikamilifu mpaka mradi kukamilika na kuwapongeza watekelezaji wa mradi huo ambao ni Ruwasa ikungi na mkoa wa singida







Share To:

Post A Comment: