**********************

VIJANA wametakiwa kuondoa wasiwasi na kutokata tamaa ambavyo kupelekea mtu kuona hawezi kutimiza malengo yake na hivyo ndoto zake kuishia njiani.

Hayo yamesemwa na Miss Pwani 2021 Agness Satura alipotembelea Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) mwishoni mwa wiki hii.

Miss Pwani huyo alipata fursa ya kukutana na kubadilishana uzoefu katika maswala ya urembo, sanaa na utamaduni na washindi wa BSS 2021, washindi wa Taifa Cup Music Challenge 2021 ambao wamekuja kujinoa zaidi katika maswala ya muziki kwa udhamini wa Wizara ya Utamaduni Sanaa na Michezo ikishirikiana na TaSUBa.

Aidha Miss Satura alikutana pia na kufanya mazoezi na vijana wenye ulemavu wa kusikia ambao wameweka kambi TaSUBa kwa ajili ya maandalizi ya mashindano ya dunia ya viziwi ya ulimbwende na utanashati.

"Ndoto ni kama malengo ambayo kila mmoja anakua amejiwekea katika maisha yake, mafanikio ni pale unapokua umeweza kutimiza ndoto zako," alisema Miss Pwani.

Miss Satura alisema kuweka ndoto yako hai na kuiishi ni kuepuka kufanya makosa ambayo wengi wanaokata tamaa huyafanya.

Miss Pwani aliwataka vijana kuwa imara wasiruhusu wasiwasi uwatale, waendelee kuweka msimamo na kushikilia malengo yao.
Share To:

emmanuel mbatilo

Post A Comment: