Diwani wa Kata ya Ipande,Edmon Mpondo (wa kwanza  kushoto) akiwa na wachezaji wa Timu ya Muhanga FC wakati wa mashindano hayo .

Wachezaji wa Timu ya Sanjaranda FC wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya kuanza kwa mchezo wa nusu fainali.
Heka heka Uwanjani zikiendelea wakati wa mashindano hayo.
Mtifuano ukiendelea Uwanjani.
Piga ni kupige baina ya timu hizo kuwania mpira zikiendelea uwanjani. (Picha zote na Jumbe Ismailly)


Na Jumbe Ismailly ITIGI  


MASHINDANO ya ligi kugombea kombe la tembo, ’’TEMBO CUP 2022’’ yanayopendelea katika Halmashauri ya Itigi, wilayani Manyoni,Mkoani Singida yameingia katika hatua ya nusu fainali,ambapo timu za Kitaraka FC,Doroto FC,Sanjaranda FC na Muhanga Fc zimefanikiwa kutinga hatua hiyo.

Katika mchezo uliopigwa katika Viwanja vya Shule ya Msngi Kitaraka,Timu ya Doroto FC ilipata goli la kuongoza katika dakika 26 lililofungwa na Karimu Mrinja na Kitaraka FC walipata goli la kusawazisha katika dakika ya 63 mfungaji akiwa Bashiru Ally na kuzifanya timu hizo kutoka sare ya kufungana goli 1 kwa 1.

Katika mchezo huo uliochezeshwa na mwamuzi Lucas Alfayo akisaidiwa na washika vibendera Marco Damasi na Paschal Mapalala,ndipo baada ya matokeo hayo mwamuzi wa mchezo huo alilazimika kutumia sheria inayozitaka timu hizo kupiga mpira ya adhabu na ndipo Daroto FC walipata kona 4 dhidi ya kona 3 za Kitaraka FC na hivyo kuiwezesha Doroto FC kutinga fainali na timu ya Muhanga FC.

Hata hivyo katika mchezo uliochezwa kwenye uwanja wa shule ya msingi Ipande uliozishirikisha timu za Muhanga FC na Smart boy FC,timu hizo zilitoka kwa sare ya kufungana goli 1 kwa 1 na hivyo kuingia kwenye hatua ya penalti na ndipo Muhanga FC waliibuka na ushindi wa jumla ya goli 3 kwa 1walilopata Sanjaranda.

Kufuatia matokeo hayo mchezo wa fainali kwa timu za Muhanga FC na Doroto FC unatarajiwa kufanyika katika uwanja wa michezo wa shule ya msingi Doroto ili kupata bingwa wa mashindano haya huku timu za Sanjaranda FC na Smart boy FC zikichuana kumpata mshindi wa tatu.

Akizungumza mara baada ya kukamilika kwa mchezo kati ya Muhanga na Smart boy,Diwani wa Kata ya Ipande,Kedmon Mpondo pamoja na mambo mengine alitumia fursa hiyo kulishukuru shirika la STEP kwa ufadhili wake wa kuandaa mashindano hayo kwa mwaka wa nne mfululizo hivi sasa pamoja na kuwasaidia kuunda vikundi vya wajasiriamali.

Diwani huyo mpenda michezo alifafanua kwamba licha ya kupatiwa elimu juu ya kuishi vizuri na mnyama tembo,vile vile watakuwa tayari kuhakikisha tembo anakuwa ni rafiki na binadamu kwa kuhakikisha anapata ulinzi wa kutosha katika maisha yake.

‘’Na sisi kama kata ya Ipande mashindano haya yametunufaisha sana kwani vijana wanakuza vipaji na hatimaye timu yetu ya Muhanga imeingia fainali na kesho itaenda kucheza Doroto.’’alisisitiza diwani huyo kijana na mpenda michezo.

Mashindano hayo yaliyozishirikisha jumla ya timu 20 kutoka katika kata zilizopo kwenye hifadhi ya Muhesi,yameandaliwa na Shirika lisilokuwa la kiserikali (STEP) limalojishughulisha na uhifadhi wa tembo nchini.


Share To:

dotto mwaibale

Post A Comment: