Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Othman Masoud Othman, leo Agosti 15, 2022, amekutana na Uongozi wa Baraza la Taifa la Watu Wenye Ulemavu kwaajili ya kuanza kusimamia utekelezaji wa shughuli za Taasisi hiyo, kwa Mwaka wa Fedha wa 2022/ 2023.


Kikao hicho ambacho ni muendelezo wa Mhe. Othman, kukutana na Taasisi zilizopo chini ya Ofisi yake, kimefanyika katika Ukumbi wa Ofisi ya Makamu wa Kwanza Migombani - Zanzibar, na kuwahusisha pia Viongozi na Watendaji mbali mbali ambao ni pamoja na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Kwanza Mhe. Harusi Said Suleiman; Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Kwanza,  Dkt. Omar Dadi Shajak; na Mkurugenzi wa Baraza la Taifa la Watu Wenye Ulemavu Zanzibar, Bw. Ussi Khamis Debe.Kitengo cha Habari

Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar

Agosti 15, 2022.

Share To:

Post A Comment: