Hai,Kilimanjaro

Madiwani wa Halmshauri ya Siha Mkoani Kilimanjaro,Wameomba kupatiwa Semina ya Kuwajengea uelewa  kuhusu Sensa ili wapakapokuwa kwenye mikutano ya Wananchi  waweze kuhamasisha zoezi hilobila kuwa na mapungufu.


Hoja hiyo ya Madiwani imetolewa kufuatia kauli ya Mkurungenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo, Upendo Mangali inayowataka madiwani hao kwenda kuhamasisha Sensa kwa Wananchi  katika maeneo yao ili wananchi waweze kutoa ushirikisano wa kutosha kwa makarani wa sensa watakapofika kwenye maeneo yao.


Baada ya kauli hiyo Madiwani hao wakizungumza kwenye kikao cha kawaida cha kuwasilisha taarifa za Kata kilichofanyika katika ukumbi wa Halmshauri hiyo,wamesema Semina hiyo ni muhimu ili kuwajengea uelewa ili wasije wakaharibu wakati wa kujibu maswali kwa Wananchi.


Mmoja wa Madiwani hao,Suzuni kihundwa wa kata ya Kashashi Wilayani humo,amesema ni vema wao kama Madiwani  wakapata Semina  ya kuwajengea uelewa japo  kwa siku mbili ,ili kuwaongea kwa Wananchi tuongee kitu kilichokuwa sahihi.


Naye Mkurungenzi Mtendaji wa Halmashari hiyo Upendo Mangali,amemesema omhi la mafunzo hayo wamelipokea lakini halitakuwa la siku mbili ambapo mara baada ya Baraza jilo kukamilia ,watapata  muongozo  na kusomewa ili wajue majukumu yao.


"Kweli baada ya mkutano huu wa kawaida wa Madiwani kumalizika atakuwepo Mtumishi atakayetoa muongozo huo wa Sansa ,kwa siku moja na sio siku mbili Kama mlivyoomba ,kwa sababu haipo kwenye Muongozo "amesema Mangali


Sambamba na haho Mkurungenzi Mtendaji wa halmashauri hiyo,amesema katika ajira za muda kweye Sensa wapo vijana 596 katika Wilaya hiyo,kati yao vijana 504 ni ajira kwa vijana wasio kuwa na ajira ambapo ajira hizi za muda zimejikitazaidi kwa vijana wasio kuwa na ajira,na sisi tumefanya hivyo,ambapo kata zipatazo 2889 zinaztarajiwa kufikiwa


Hata hivyo madiwani hao walifakiwa kupata semini ya muda mfupi kutoka Mkufunzi mkuu wa Sensa Wilaya ya Siha kutoka Ofisi ya Takwimu,Husen Mavunde,ambapo madiwani hao walishukuru.

Share To:

JUSLINE

Post A Comment: