MENEJA wa Bidhaa wa LG Afrika Mashariki Eden Seo (kushoto), akiwa na Mkurugenzi Mkuu wa LG Afrika Mashariki, Sa Nyoung Kim na Mkurugenzi Mkuu wa Opalnet Rakesh Singh, wakati wa uzinduzi wa friji mpya za LG zenye punguzo la asilimia 33 katika kipindi cha mwezi mzima wa kusherekea sikukuu ya Nane Nane jana jijini Dar es Salaam.


Meneja Mauzo Kampuni ya LG East Africa- GARNET STAR- Bi. Nancy Mhagama akimuonyesha mmoja wa wateja mashine ya kufulia katika Duka la LG GARNET STAR  jijini Dar es Salaam, Tanzania. Mashine ya kuosha ya AI DD ni mojawapo ya vifaa mahiri vya LG ambavyo havigundui uzito tu bali pia huhisi ulaini wa kitambaa, na huchagua ni njia bora ya kusafisha kitambaa husika bila kuleta madhara. LG Electronics East Africa pamoja na muungano wa GARNET STAR kwa sasa inatoa punguzo la hadi 33% kwa bidhaa mahususi kwa Watanzania hadi tarehe 28 Agosti 2022.

Mameneja  Mauzo wa LG East Africa Brandshop GARNET STAR Khadija Issa (kushoto) na Nancy Mhagama (kulia) wakiwa  na mteja aliyekuja kununua bidhaa katika duka la  GARNET STAR LG jijini Dar es Salaam, Tanzania.

............................................................................................................................................................

Na Mwandishi Wetu.

KAMPUNI ya vifaa vya umeme Afrika Mashariki ya LG kwa kushirikiana na Garnet Star, imetoa ofa ya punguzo ya asilimia 33 kwa bidhaa zake kwa Watanzania, katika kipindi cha mwezi huu wa Sikukuu ya Nane Nane.

Promosheni hiyo inatarajiwa kufikia ukomo Agosti 28 mwaka huu ambapo wateja watapata fursa ya kuokoa kuanzia asilimia 10 hadi asilimia 33 ya manunuzi ya bidhaa za LG katika maduka ya Garnet Star ikiwa ni sehemu ya kusherehekea mwezi wa sikukuu ya Nane Nane nchi nzima.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam , Mkurugenzi Mtendaji wa LG kwa Afrika Mashariki, Sa Nyoung Kim alisema , “Wakulima wapo kwa ajili ya kutupatia chakula sisi na taifa zima kwani kila mwaka tunasherehekea hii sikukuu ya Nane Nane.

“Tumeamua kusherekea nao katika sikukuu hii kwa kuwawekea punguzo la bei katika bidhaa zetu kwa kipindi hichi hadi Agosti 28, mwaka huu.

“Sisi kama LG, tumejiwekea mikakati ya kuendelea kuwa pamoja na wakulima na kuwaletea bidhaa mbalimbali zenye ubora zaidi ili kuendeleza ushindani sokoni,” alisema.

Alisema mteja atapata nafasi punguzo la asilimia kuanzia 10 hadi 33, lakini inategemea na bidhaa za umeme za nyumbani atakazonunua.

Vifaa mbalimbali vimeingia katika punguzo hilo vikiwemo viyoyozi, friji, vifaa vya muziki na TV.

Share To:

Adery Masta

Post A Comment: