Mkuu wa Wilaya ya Rufiji Mkoani Pwani Meja Edward Gowele amesema hayo alipokuwa akitembelea maonyesho ya nanenane kanda ya mashariki yaliyofanyika mkoani morogoro ambapo amesema sekta za kilimo, ufugaji na uvuvi vinatakiwa kufuata ushauri wa wataalamu vita weza kupunguza migogoro katika ya wakulima na wafugaji.
Meja Gowele amesema kuwa kupitia maonyesho ya nanenane wataweza kujifunza Teknolojia mpya zinavyo badilishwa kutoka kwenye kilimo cha mkono na kwenda kwenye kilimo cha kisasa ambacho ndio kilimo chenye tija na kumnufaisha mkulima .
Pia amesema kuwa katika maonyesho hayo wameona namna wafugaji wanavyofuga mifugo kwa njia ya kisasa na kwanjia nzuri za kunenepesha wanyama kwa kutumia malisho bora kwa kupanda majiani ambayo yatasaidia kuepusha migogoro katika ya wakulima na wafugaji iliyopo sasa katik maeneo mengi.
Aidha Mkuu wa Wilaya Meja Edward Gowele amesema kama elimu hii ya kilimo ,ufugaji na uvuvi itafika vizuri Kwa watanzania kutakuwa na mabadiliko makubwa kwani sekta hizo muhimu ambapo zitakuwa na tija kwa wakulima wavuvi na wafugaji wataweza kufanya shughuli zao kibiashara na kuweza kupata mafanikio yao na taifa litaweza kunufaika.
Post A Comment: