Na Esther Macha,


KUNA msemo usemao ukimuwezesha mwanamke, umeiwezesha jamii, msemo huu licha ya ukweli wake mara nyingi hautiliwi maanani na juhudi za kutekelezeka l kubwa na changamoto mbali mbali za kijamii, kitamaduni au kiuchumi.


Dhana hii imemfanya mwanamke kuwa na juhudi za kufanya kazi na hata kujituma kwenye shughuli za ujasiliamali mbali mbali ili waweze kujiongezea kipato katika maisha maisha yao.


Kutokana na msukumo wa uwezeshaji kiuchumi kwa wanawake kuwa nguzo muhimu kwao na kuachana na dhana ya kuwa tegemezi kwa waume zao ,tofauti ya miaka ya nyuma ambapo wanawake walikuwa watu wa kukaa nyumbani tu na kusubiri kulea familia .


Lakini sera ya wanawake ni wajowapo ya miongozo ya serikali katika jitihada za kuwapa wananchi mwelekeo wa maendeleo ya wanawake na jinsia ambayo itahakikisha kuwa sera,mipango mikakati na shughuli mbali mbali za maendeleo katika kila sekta na taasisi ngazi zote zinazozingatia usawa wa jinsia.


Akizungumza na gazeti hili Katibu umoja wa wanawake wilaya ya Chunya na Diwani wa vitimaalum kata ya Mkwajuni ,Zaitun Sembo anasema kuwa katika kuhakikisha kuwa wanawake wanaondokana na hali duni na kuachana na hali ya kuwa tegemezi tayari kila mwanamke sasa ana uchumi wake mwenyewe.


Sembo anasema kuwa wanamshukuru Mbunge wa vitimaalum na Naibu waziri wa maji , Mhandisi Maryprisca Mahundi kwa jinsi anavyopambana kuwakwamua wanawake wa wilaya zote za mkoa wa Mbeya ili kila mmoja awe mjasiliamali anayejitegemea.


“Tunashukuru sana kwani mpaka kila mwanamke amepatiwa mtaji wa shilingi laki moja ili aweze kujishughulisha na biashara mbali mbali kwa wilaya zote za mkoa wa Mbeya hii kwetu jambo la faraja sana kwani tunajua fedha hizi angeweza kupeleka kwenye familia yake lakini akaona ni vema kuwainua wanawake wa mkoa wa Mbeya kiuchumi”anasema Sembo.


Akielezea zaidi Sembo anasema kwamba mbali na kutoa mitaji hiyo kwa wanawake wote wa mkoa huo Mhandisi Mahundi pia alikabidhi majiko 500 ya gesi kwa wilaya zote za mkoa wa Mbeya ambapo kila mwanamke alipatiwa jiko la gesi .


Lengo la kutoa majiko hayo kwa wanawake ni kuweza kuwasaidia ili kuondokana na uharibifu wa mazingira na badala yake kutumia majiko ya gesi ili kuendelea kukabiliana na uharibifu wa mazingira .


Sophia Mwanautwa ni Diwani wa vitimalaam kata ya Makongorosi anasema kuwa wanawake wa wilaya ya chunya kwasasa wameweza kuwa na uchumi mzuri wa kipato na hata kusomesha watoto wao kutokana na kupatiwa mitaji ya kuendeleza biashara zao na hata ambao hawakuwa na biashara wameweza kuanzisha ujasiliamali mdogo ambao mpaka sasa umeweza kuwainua katika kipato na kuondokana na hali duni ya kimaisha.


Mwanautwa anasema kuwa mbunge wa vitimalaam na Naibu waziri wa maji mhandisi mahundi amekuwa msaada kuwa kwa wanawake wa mkoa wa mbeya na kwamba hivi sasa hakuna mwanamke ambaye anakaa bure pasipo kujishughulisha kutokana na kupewa kianzio cha mtaji wa biashara ili aweze kujikwamua kimaisha.


“Tunaamini wapo viongozi wengi ambao wanaweza kumkwamua mwanamke ila naona kujitoa ndo huwa changamoto kubwa hivyo alinachofanya Mbunge huyu inabidi sisi wanawake tusimwangusha kwa hiki kianzio cha mitaji alichotupa,lakini bado ametuwezesha mashine ya kusagia mawe ya dhahabu (Kalasha) lenye thamani ya shilingi mil.10 hili jambo la kushukuru sana tunamwombea heri Mbunge wetu”anasema Mwanautwa.


Aidha Mwanautwa anasema kuwa katika wilaya ya Chunya wana ujenzi wa nyumba ya Katibu wa umoja wanawake wilayani humo ambao ndo umeanza upo kwenye hatua za awali ,Mbunge huyo wa vitimaluum aliweza kuchangia shilingi laki tano ili ziweze kusaidia kuwalipa mafundi pamoja na kukabidhi vifaa vya ujenzi.


Mbunge wa viti maluum mkoa wa Mbeya


Akizungumza hivi karibuni akiwa wilayani humo kwa ziara ya kichama Mbunge wa vitimaluum Mkoa wa Mbeya na Naibu wa waziri wa maji Mhandisi Maryprisca mahundi anasema kuwa moyo wake moyo wake unawaza mambo makubwa kwa wanawake wa mkoa wa Mbeya ,


“Mimi nilitoa ahadi ya mashine ya kusaga mawe ya dhahabu (Karasha) kama mradi wa awali kwa umoja wa wanawake na nimekamilisha sasa wanawake wanaenda kumiliki mradi mkubwa na nashukuru Mungu nimekamilisha ahadi yangu kwa wanawake wilaya hii ,tumeanza miradi hii ya maendeleo tarajieni mambo makumbwa zaidi ,nashukuru mungu nilisema lazima nyumba ya katibu lazima ikamilike nashukuru sana sasa ujenzi wa nyumba ya inaenda kukamilika na kuwa mfano kwa kuwa na nyumba bora ya Katibu”anasema.


Mhandisi Mahundi anasema Karasha hilo lina thamani ya zaidi ya mil.9


Hata hivyo Mhandisi Mahundi anasema kuwa mpango wake wa maendeleo kwa kiwilaya za mkoa wa Mbeya unatekelezeka kwa wanawake wote ili kila mmoja aweze kuwa na uchumi wake ambao utamfanya ajitegemee na kuondokana hali ya kutokuwa tegemezi.


Kwa upande katibu wa chama cha mapinduzi wilaya ya Chunya ,Charles Jokeli alimshukuru Mbunge huyo na Naibu waziri wa` maji kwa kuwakomboa wanawake wilayani humo kwa kukabidhi mradi mkubwa ambao utawakomboa kiuchumi .


Aidha Jokeli anasema kuwa pia Mbunge huyo amsema mbunge huyo amekuwa kinara katika kuwaletea maendeleo wanawake pia ameweza kukabidhi majiko ya gesi kwa wanawake wilayani humo ili waweze kujikomboa ,katika sakata` la kitaifa la programu ya chama Taifa kuwa kila wilaya ijenge nyumba ya katibu Mbunge huyo amekuwa mfano wa kuwezesha ujenzi wake kuanza .


“Leo hii tumeshuhudia tukio kubwa la kukabidhi mradi huu mkubwa kwa wanawake wa wilaya hii ,ni matumaini yetu kuwa mradi huu utasonga mbele lakini ili uende mbele unahitaji usimamizi mkubwa na uaminifu naamini kamati ya utekelezaji wilaya itasimamia kwa kikamilifu, mradii huu ambao unaenda kuwa mkombozi kwa wanawake wa wilaya hii kiuchumi “anasema Katibu wa chama mapinduzi Wilaya.


 


Ugawaji wa majiko ya gesi na` Mitaji kwa umoja wa wanawake (UWT)



Hata hivyo Mbunge huyo wa viti maalum mkoa wa Mbeya na Naibu waziri wa maji Mhandisi ,Maryprisca Mahundi pamoja kufungua miradi ya kiuchumi kwa baadhi ya wilaya pia ameweza kuwawezesha wanawake majiko ya gesi ili waweze kuondokana na matumizi ya mkaa ili kutunza mazingira katika maeneo yao.


Aidha Mhandisi Mahundi anasema kuwa akiwa kama Naibu waziri wa maji anapenda kuona kuwa mazingira yanatunzwa na kupenda utamaduni wa kuona kuwa kila mwananchi anakuwa rafiki wa mazingira na wizara ya maji wanajitahidi kuwa rafiki wa kutunza mazingira.


 


Akelezea zaidi Mhandisi Mahundi anasema kuwa wanawake ndo watunzaji wa mazingira namba moja na wanawake ndo waandaji wa chakula katika familia na kwamba wanawake walio wengi wapo nje ya mji ambao asimilia kubwa wanatumia kuni pamoja na mkaa.


 


"Dhamira ya kuona hii kampeni ya kupunguza matumizi ya mkaa na kuni na kuwaingiza wanawake kwenye mwamko na kuona kuwa wanawake wanaweza kutumia gesi Kama nishati mbadala namshukuru sana mkurugenzi mkuu wa Oryx kwa kukubaliana na mawazo yangu mimi mwakilishi wa wanawake Mkoa wa mbeya"anasema Mhandisi Mahundi.


Hata hivyo Naibu waziri wa maji anasema kuwa wanaenda kuanza zoezi la kukabidhi majiko ya gesi 500 wanawake hao wanakwenda kuwapata kote za mkoa wa mbeya na majimbo yote na kuwa kila wila atagawa majiko ya gesi 50.


Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Oryx Tanzania ,Araman Benoit anasema kuwa baada ya kupokea maombi kutoka kwa Naibu waziri wa maji Mhandisi Mahundi wanaungana nae katika kampeni ya utunzaji mazingira na hivi sasa huduma yao gesi ya Oryx inapatikana mpaka vijijini.


Aidha Mhandisi Mahundi anasema kuwa katika kuhakikisha kuwa kila mwanamke anakuwa na uchumi wake ameweza kukabidhi fedha za mitaji kila mwanamke ili waweze kufanya shughuli za ujasiliamali ambao utawafanya kuachana na hali ya kuwa tegemezi.




Oliver Kibona ni Mwenyekiti umoja wa wanawake mkoa wa Mbeya (UWT) anasema kuwa hivi sasa wanawake wamekuwa wa kujiamini kutokana na kila mmoja kuwa na uchumi wake ambao unamwezesha kuendesha maisha yake bila hofu.


Kibona anasema kuwa uwezeshaji kiuchumi ambao umefanya Mbunge wa viti maalum mkoa wa Mbeya , Mhandisi Maryprisca Mahundi umeleta ari kubwa kwa wanawake kufanya kazi kwa kujituma na hata miradi iliyoanzishwa na umoja huo inasonga mbele zaidi na kuwapa moyo wa kujituma na kusimamia vema.



Share To:

Post A Comment: