Wananchi wa Msomera Wilayani Handeni waliohama kwa hiyari kutoka Wilayani Ngorongoro Mkoani Arusha wamempongeza Mkuu wa Wilaya hiyo Mheshimiwa Siriel Mchembe kwa kuwapokea na kuwapa ushirikiano katika mambo mbalimbali ya kimaendeleo.


Pongezi hizo zimetolewa na wananchi hao katika hafla fupi iliyofanywa na wazee wa kimila na Malaigwanak (machief) wa jamii ya kimaasai ambapo kwa pamoja wamempa jina jipya mkuu huyo wa wilaya la Namelok sambamba zawadi ya Ng'ombe jike.

Pia Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya na Katibu wa Chama Cha Mapinduzi CCCM) Wilaya Bi. Anastazia Amas wamepewa  zawadi na wananchi hao kwa kazi nzuri kwa kusimamia zoezi hilo kikamilifu na kwa mafanikio makubwa.

Aidha Wananchi hao wamebadilishana mifugo ili kuimarisha undugu sawasawà na mila yao ya Kimaasai ambapo zoezi hilo limesimamiwa na Machief wa kimaasai sambamba na viongozi wa dini.

Hayo yamejiri baada ya kufanyika kikao cha Halmashauri Kuu ya Kijiji na Mkutano Mkuu Maalum wa Kijiji ambapo Wazee hao wa Kimaasai na Malaigwanak (machief)  wameshukuru kwa kufanikisha kuwaunganisha wana Ngorongoro na wana Msomera na kusimamia vizuri zoezi zima na Msomera. 

Hafla hiyo imehitimishwa kwa kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuifanya Msomera kuwa nchi iliyobarikiwa kama Kanaani sambamba hilo pia amemshukuru Waziri Mkuu Mheshimiwa Kassim Majaliwa pamoja na wasaidizi wake.


Kwa upande wa wafugaji hao wakiwakilishwa na Mwenyekiti wa wafugaji Taifa Ndg.Jeremia na Katibu wa wafugaji Taifa Walitoa elimu ya ufugaji na kuwaasa Wamaasai kuacha kuzunguka na mifugo bali wafuge mifugo yao kwa njia ya kisasa ili kuweza kupata faida nyingi.



















Share To:

Post A Comment: